Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 16:34 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

34 Akawaleta juu nyumbani kwake, akawaandalia, akafurahi sana, yeye na nyumba yake yote, maana amekwisha kumwamini Mungu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

34 Halafu akawachukua Paulo na Sila nyumbani kwake, akawapa chakula. Yeye na jamaa yake yote wakafanya sherehe kwa vile sasa walikuwa wanamwamini Mungu].

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

34 Halafu akawachukua Paulo na Sila nyumbani kwake, akawapa chakula. Yeye na jamaa yake yote wakafanya sherehe kwa vile sasa walikuwa wanamwamini Mungu].

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

34 Halafu akawachukua Paulo na Sila nyumbani kwake, akawapa chakula. Yeye na jamaa yake yote wakafanya sherehe kwa vile sasa walikuwa wanamwamini Mungu].

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

34 Akawapandisha nyumbani mwake akawaandalia chakula, yeye pamoja na nyumba yake yote wakafurahi sana kwa kuwa sasa walikuwa wamemwamini Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

34 Akawapandisha nyumbani mwake akawaandalia chakula, yeye pamoja na nyumba yake yote wakafurahi sana kwa kuwa sasa walikuwa wamemwamini Mwenyezi Mungu.

Tazama sura Nakili




Matendo 16:34
26 Marejeleo ya Msalaba  

Tena kufanya furaha na kuona furaha kulikuwa wajib, kwa maana huyu ndugu yako alikuwa amekufa, nae amefufuka: alikuwa amepotea, nae ameonekana.


Akashuka upesi, akamkaribisha kwa furaha.


Nae Lawi akamfanyia karamu kubwa nyumbani mwake: na palikuwa na kundi kubwa la watoza ushuru, na watu wengine waliokuwa wameketi pamoja nao chakulani.


atakaekuambia maneno ambayo utaokolewa nayo, wewe na nyumba yako yote.


Hatta alipokwisha kumbatiza, yeye na nyumba yake, akatusihi, akisema, Kama mmeniona kuwa mwaminifu kwa Bwana, ingieni nyumbani mwangu mkakae; akatushurutisha.


Kulipopambazuka makadhi wakawatuma wakubwa wa askari wakisema, Waacheni watu wale waende zao.


Na siku zote kwa moyo mmoja walidumu ndani ya hekalu, wakimega mkate nyumba kwa nyumba, na kupokea chakula chao kwa furaha na kwa moyo mweupe,


Kiisha, walipotoka majini, Roho ya Bwana ikamnyakua Filipo, yule tawashi asimwone tena; maana alikwenda zake akifurahi:


Bassi Mungu wa tumaini awajazeni furaha yote na amani katika kuamini, mpate kuzidi sana kuwa na tumaini, katika nguvu za Roho Mataktifu.


Wala si hivyo tu, illa na twajifurahisha katika Mungu kwa Bwana wetu Yesu Kristo ambae kwa yeye tuliupokea upatanisho.


kwa yeye tumepata kwa njia ya imani kuifikia neema hii ambayo tunasimama ndani yake; na twafurahi katika tumaini la utukufu wa Mungu.


Lakini matunda ya Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,


Si kwamba nakitamani kile kipawa, bali nayatamani mazao yanayozidi kuwa mengi, katika hesabu yenu.


Furahini katika Bwana siku zote; marra ya pili nasema, Furahini.


Maana tuna furaha na faraja kwa sababu ya upendo wako, kwa kuwa mioyo ya watakatifu lmeburudishwa nawe, ndugu.


Watoto, tusipende kwa neno, wala kwa ulimi, biali kwa tendo na kweli.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo