Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Matendo 16:26 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

26 Ghafula pakawa tetemeko kuu la inchi, hatta misingi ya gereza ikatikisika, na marra hiyo milango ikafunguka, vifungo vya watu wote vikalegezwa.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

26 Ghafla, kulitokea mtetemeko mkuu wa ardhi ambao uliitikisa misingi ya gereza. Mara, milango yote ikafunguka na minyororo iliyowafunga hao wafungwa ikaachana.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

26 Ghafla, kulitokea mtetemeko mkuu wa ardhi ambao uliitikisa misingi ya gereza. Mara, milango yote ikafunguka na minyororo iliyowafunga hao wafungwa ikaachana.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

26 Ghafla, kulitokea mtetemeko mkuu wa ardhi ambao uliitikisa misingi ya gereza. Mara, milango yote ikafunguka na minyororo iliyowafunga hao wafungwa ikaachana.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

26 Ghafula pakatokea tetemeko kubwa la ardhi, hata msingi wa gereza ukatikisika. Mara milango ya gereza ikafunguka na ile minyororo iliyowafunga kila mmoja ikafunguka.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

26 Ghafula pakatokea tetemeko kubwa la ardhi, hata msingi wa gereza ukatikisika. Mara milango ya gereza ikafunguka na ile minyororo iliyowafunga kila mmoja ikafunguka.

Tazama sura Nakili

Matendo 16:26
15 Marejeleo ya Msalaba  

Na kumbe! palikuwa na tetemeko kubwa la inchi; kwa sababu malaika wa Bwana alishuka mbinguni, akakaribia akalifingirisha lile jiwe mbali ya mlango, akaketi juu yake.

Na walipopita lindo la kwanza na la pili, wakaja hatta mlango wa chuma wa kuingilia mjini, ukawafungukia. Wakatoka, wakapita katika njia moja; marra malaika akamwacha.

Marra malaika wa Bwana akasimama karibu nae, nuru ikamulika chumbani mle, akampiga Petro ubavuni, akamwamsha, akisema, Ondoka upesi. Minyororo ikamwanguka.

Hatta walipokwisha kumwomba Mungu, pahali paie walipokusanyika pakatikiswa, wote wakajaa Roho Mtakatifu, wakanena neno la Mungu kwa uthabiti.

lakini malaika wa Bwana akafungua milango ya gereza usiku, akawatoa, akasema,

Na katika saa ile palikuwa na tetemeko la inchi, nalo kubwa, na sehemu ya kumi ya mji ikaanguka, wana Adamu elfu saba wakauawa katika tetemeko lile. Na waliosalia wakaingiwa na khofu wakamtukuza Mungu wa mbingu.

Nikaona, alipoifungua muhuri ya sita, tazama, palikuwa tetemeko kuu la inchi, jua likawa jeusi kama gunia la nywele, mwezi ukawa kama damu,

Tufuate:

Matangazo

Matangazo