Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 16:25 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

25 Lakini panapo usiku wa manane Paolo na Sila walikuwa wakimwomba Mungu na kumwimbia nyimbo za kumsifu, na wafungwa wengine walikuwa wakisikiliza.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

25 Karibu na usiku wa manane Paulo na Sila walikuwa wakisali na kuimba nyimbo za kumsifu Mungu, huku wafungwa wengine wakiwa wanasikiliza.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

25 Karibu na usiku wa manane Paulo na Sila walikuwa wakisali na kuimba nyimbo za kumsifu Mungu, huku wafungwa wengine wakiwa wanasikiliza.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

25 Karibu na usiku wa manane Paulo na Sila walikuwa wakisali na kuimba nyimbo za kumsifu Mungu, huku wafungwa wengine wakiwa wanasikiliza.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

25 Ilipokaribia usiku wa manane, Paulo na Sila walikuwa wakiomba na kuimba nyimbo za kumsifu Mungu, nao wafungwa wengine walikuwa wakiwasikiliza.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

25 Ilipokaribia usiku wa manane, Paulo na Sila walikuwa wakiomba na kuimba nyimbo za kumsifu Mungu, nao wafungwa wengine walikuwa wakiwasikiliza.

Tazama sura Nakili




Matendo 16:25
38 Marejeleo ya Msalaba  

Nae kwa kuwa alikuwa na huzuni sana, akazidi kuomba kwa bidii. Hari yake ikawa kama matone ya damu yakidondoka hatta inchi.


Bassi ikawapendeza mitume na wazee na Kanisa lote kuwachagua watu miongoni mwao na kuwapeleka Antiokia pamoja na Paolo na Barnaba: nao ni hawa, Yuda aliyekwitwa Barsaba, na Sila, watu wakuu katika ndugu.


Bassi bwana zake walipoona ya kuwa tumaini la faida yao limewapotea, wakawakamata Paolo na Sila, wakawakokota hatta sokoni mbele ya wakuu wa mji;


Akawakaribisha saa ile ile ya usiku, akawaosha mapigo yao, akahatizwa, yeye ua watu wote wa nyumbani mwake wakati huohuo.


Nao wakatoka katika ile baraza, wakifurahi kwa sababu wamehesabiwa kuwa wamestahili kuaibishwa kwa ajili ya jina lake.


kwa tumaini, mkifurahi; katika shidda, mkivumilia; katika kusali, mkidumu;


Wala si hivyo tu, illa twafurahi katika mateso pia, tukijua ya kuwa dhiiki, kazi yake ni kuleta uvumilivu,


kama wenye huzuni, bali siku zote wenye furaha; kama maskini, bali tukitajirisha wengi; kama wasio na kitu, bali wenye vitu vyote.


mkisemezana kwa zaburi na fenzi na nyimbo za roho, mkiimba na kumshangilia Bwana mioyoni mwenu;


Naam, hatta nikimiminwa juu ya dhabihu na khuduma ya imani yenu, nafurahi; tena nafurahi pamoja nanyi nyote.


Sasa nayafurahia mateso niliyo nayo kwa ajili yenu; tena natimiliza yale yaliyopungua ya mateso ya Kristo katika mwili wangu, kwa ajili ya mwili wake, yaani, kanisa lake,


Yeye siku hizo za niwili wake alimtolea yeye awezae kumwokoa na kumtoa katika mauti, maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi, akasikilizwa kwa sababu ya kicho chake;


Hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, ndugu zangu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali;


Mtu wa kwenn amepatikana na mabaya? na aombe. Ana moyo wa kuchangamka? na aimbe zaburi.


Mkilaumiwa kwa ajili ya jina la Kristo ni kheri yenu, kwa kuwa Roho ya utukufu na ya Mungu unawakalia; kwa hawo anatukanwa, bali kwenu ninyi anatukuzwa.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo