Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 16:23 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

23 Na walipokwisha kuwapiga mapigo mengi, wakawatupa gerezani, wakamwamuru mlinzi wa gereza awalinde sana.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

23 Baada ya kupigwa sana wakatiwa ndani, na askari wa gereza akaamriwa kuwaweka chini ya ulinzi mkali.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

23 Baada ya kupigwa sana wakatiwa ndani, na askari wa gereza akaamriwa kuwaweka chini ya ulinzi mkali.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

23 Baada ya kupigwa sana wakatiwa ndani, na askari wa gereza akaamriwa kuwaweka chini ya ulinzi mkali.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

23 Baada ya kuwapiga sana, wakawatupa gerezani na kumwagiza mkuu wa gereza awalinde kikamilifu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

23 Baada ya kuwachapa sana, wakawatupa gerezani na kumwagiza mkuu wa gereza awalinde kikamilifu.

Tazama sura Nakili




Matendo 16:23
21 Marejeleo ya Msalaba  

Na yeye anaemsaliti amewapa ishara, akinena, Nitakaembusu, ndiye; mkamateni.


Lakini kabla ya haya yote watawakamateni na kuwaudhini, watawapelekeni mbele ya sunagogi na gerezani, mkichukuliwa mbele ya wafalme na maliwali kwa ajili ya jina langu.


Hatta kulipopambazuka askari wakaingiwa na fadhaa nyingi, amekuwaje Petro.


Alipokwisha kumkamata, akamweka gerezani akamtia mikononi mwa askari wanewane, wamlinde, akitaka baada ya Pasaka kumtoa mbele ya watu.


Yule mlinzi wa gereza akaamka, akaona ya kuwa milango ya gereza imefunguka, akafuta upanga wake, akataka kujiua, akidhani ya kuwa wafungwa wamekimbia.


Yule mlinzi wa gereza akamwarifu Paolo maneno haya ya kama, Makadhi wametuma watu kuwafungulieni! bassi, sasa tokeni nje, enendeni zenu kwa amani.


wakawakamata mitume wakawaweka ndani ya gereza;


wakarudi wakatoa khabari, wakisema, Gereza tumeikuta imefungwa salama salamini, nao walinzi wamesimama mbele ya mlango: lakini tuliponfungua hatukukuta mtu ndani.


Saul akaliharibu kanisa, akiingia killa nyumba, na kuwabarura wanaume na wanawake na kuwatupa gerezani.


akataka ampe khati za kwenda Dameski zilizoandikwa kwa masunagogi, illi akiona watu wa Njia hii, waume kwa wake, awafunge na kuwaleta Yerusalemi.


Wao wakhudumu wa Kristo? (nanena kiwazimu), mimi zaidi; kwa kazi kuzidi sana; kwa mapigo kupita kiasi; kwa vifungo kuzidi sana; kwa mauti marra nyingi.


kafika mapigo, katika vifungo, katika fitina, katika kazi, katika kukesha, katika kufunga;


KWA sababu biyo mimi Paolo, mfungwa wake Kristo Yesu kwa ajili yenu ninyi Mataifa,—


BASSI nawasihini, mimi niliye mfungwa katika Bwana, mwenende kama inavyoustahili wito wenu mlioitiwa,


Katika huyu nimeteswa kiasi cha kufungwa, kama mtenda mabaya; illakini neno la Mungu halifungwi.


illakini, kwa ajili ya upendo, nakusihi, kwa kuwa ni kama nilivyo, Paolo mzee, na sasa mfungwa wa. Yesu Krlsto pia.


Mimi Yohana, ndugu yenu na mwenye kushiriki pamoja nanyi katika mateso na ufalme na uvumilivu wa Yesu Kristo, nalikuwa katika kisiwa kiitwacho Patmo, kwa ajili ya Neno la Mungu, na kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu.


Usiogope mambo yatakavokupata: tazama mshitaki atawatupa baadhi yenu gerezani illi mjaribiwe, nanyi mtakuwa na mateso siku kumi. Uwe mwaminifu hatta kufa, nami nitakupa taji ya uzima.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo