Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 16:20 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

20 wakawachukua kwa makadhi, wakasema, Watu hawa wanataharakisha mji wetu, nao ni Wayahudi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

20 Wakawashtaki kwa mahakimu wakisema, “Watu hawa ni Wayahudi na wanafanya fujo katika mji wetu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

20 Wakawashtaki kwa mahakimu wakisema, “Watu hawa ni Wayahudi na wanafanya fujo katika mji wetu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

20 Wakawashtaki kwa mahakimu wakisema, “Watu hawa ni Wayahudi na wanafanya fujo katika mji wetu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

20 Baada ya kuwafikisha mbele ya mahakimu wakawashtaki wakisema, “Hawa watu wanaleta ghasia katika mji wetu, nao ni Wayahudi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

20 Baada ya kuwafikisha mbele ya mahakimu wakawashtaki wakisema, “Hawa watu wanaleta ghasia katika mji wetu, nao ni Wayahudi.

Tazama sura Nakili




Matendo 16:20
14 Marejeleo ya Msalaba  

Mfalme Herode aliposikia haya, akafadhaika, na Yerusalemi pia pamoja nae.


Bassi bwana zake walipoona ya kuwa tumaini la faida yao limewapotea, wakawakamata Paolo na Sila, wakawakokota hatta sokoni mbele ya wakuu wa mji;


Tena wanatangaza khabari ya desturi zisizo halali kwetu tuzipokee wala kuzifuata, kwa kuwa sisi tu Warumi.


Akamwona Myahudi mmoja, jina lake Akula, mzalia wa Ponto; nae amekuja kutoka inchi ya italia siku za karibu, pamoja na Priskilla mkewe, kwa sababu Klaudio amewaamuru Wayahudi wote watoke Rumi.


Lakini walipotambua ya kuwa yeye ni Myahudi, wakapiga kelele wote pia kwa sauti moja kwa muda wa saa mbili au karibu, wakilia, Artemi wa Waefeso ni mkuu.


Lakini tunataka kusikia kwako uonavyo wewe; kwa maana katika khabari za madhehebu hiyo tumekwisha kujua kwamba inanenwa vibaya kilia mahali.


Wala msifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufunya upya nia zenu, mpate kujua kwa hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.


Enyi wazinzi, wanaume na wanawake, hamjui ya kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu? bassi killa atakae kuwa rafiki wa dunia ajifanya kuwa adui wa Mungu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo