Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 16:19 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

19 Bassi bwana zake walipoona ya kuwa tumaini la faida yao limewapotea, wakawakamata Paolo na Sila, wakawakokota hatta sokoni mbele ya wakuu wa mji;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

19 Matajiri wa yule msichana walipoona kwamba tumaini lao la kupata mali limekwisha, waliwakamata Paulo na Sila, wakawaburuta mpaka hadharani, mbele ya wakuu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

19 Matajiri wa yule msichana walipoona kwamba tumaini lao la kupata mali limekwisha, waliwakamata Paulo na Sila, wakawaburuta mpaka hadharani, mbele ya wakuu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

19 Matajiri wa yule msichana walipoona kwamba tumaini lao la kupata mali limekwisha, waliwakamata Paulo na Sila, wakawaburuta mpaka hadharani, mbele ya wakuu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

19 Basi mabwana wa yule mjakazi walipoona kuwa tumaini lao la kuendelea kujipatia fedha limetoweka, wakawakamata Paulo na Sila wakawaburuta hadi sokoni mbele ya viongozi wa mji.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

19 Basi mabwana wa yule mtumwa wa kike walipoona kuwa tumaini lao la kuendelea kujipatia fedha limetoweka, wakawakamata Paulo na Sila wakawaburuta mpaka sokoni mbele ya viongozi wa mji.

Tazama sura Nakili




Matendo 16:19
24 Marejeleo ya Msalaba  

Wakati huo watawasaliti ninyi mpate kuteswa, na watawaua; na mtakuwa watu wa kuchukiwa na mataifa vote kwa ajili ya jina langu.


Nanyi jihadharini nafsi zenu; maana watawapelekeni maharazani: na katika masunagogi mtapigwa: na mtachukuliwa mbele za maliwali na wafalme kwa ajili yangu, kuwa ushuhuda kwao.


Wayahudi wakalika toka Antiokia na Ikonio, wakawashawishi makutano hatta wakampiga mawe Paolo wakamhurura nje ya mji, wakidhani ya kuwa amekwisha kufa.


Hatta palipotokea shambulio la watu wa mataifa na Wayahudi pamoja na wakubwa wao juu yao, kuwatenda jeuri na kuwapiga mawe,


Bassi ikawapendeza mitume na wazee na Kanisa lote kuwachagua watu miongoni mwao na kuwapeleka Antiokia pamoja na Paolo na Barnaba: nao ni hawa, Yuda aliyekwitwa Barsaba, na Sila, watu wakuu katika ndugu.


watu waliokhatirisha maisha zao kwa ajili ya jina la Bwana wetu Yesu Kristo.


Paolo akamchagua Sila akaondoka, akiombewa na wale ndugu, apewe neema ya Mungu.


Ikawa tulipokuwa tukienda mahali pale pa kuombea, kijakazi kimoja aliyekuwa na pepo ya Puthoni akatukuta, aliyewapatia bwana zake faida nyingi kwa kutabiri.


wakawachukua kwa makadhi, wakasema, Watu hawa wanataharakisha mji wetu, nao ni Wayahudi.


Lakini panapo usiku wa manane Paolo na Sila walikuwa wakimwomba Mungu na kumwimbia nyimbo za kumsifu, na wafungwa wengine walikuwa wakisikiliza.


Akataka taa ziletwe, akarukia ndani, akitetemeka kwa khofu, akawaangukia miguu Paolo na Sila;


na wasipowakuta, wakamkokota Yason na baadhi ya ndugu mbele ya wakubwa wa mji, wakipiga kelele, wakisema, Watu hawa walioupindua ulimwengu wamefika na huku,


Mji wote ukataharuki, watu wakakutanika mbio mbio, wakamkamata Paolo, wakamwokota, wakamtoa hekaluni; marra milango ikafungwa.


Saul akaliharibu kanisa, akiingia killa nyumba, na kuwabarura wanaume na wanawake na kuwatupa gerezani.


Maana nitamwonyesba mambo mengi makuu yatakayompasa kuteswa kwa ajili ya Jina langu.


kafika mapigo, katika vifungo, katika fitina, katika kazi, katika kukesha, katika kufunga;


mkiwa na mashindano yale yale mliyoyaona kwangu, mkasikia kvvamba ninayo hatta sasa.


bali tukiisha kuteswa kwanza na kutendwa jeuri, kama mjuavyo, katika Filippi, twalithubutu katika Mungu kuinena Injili ya Mungu kwenu, kwa kuishindania sana.


Maana shina moja la mabaya yote ni kupenda fedha, ambayo wengine wakiitamani hiyo wamefarakana na Imani na kujichoma kwa maumivu mengi.


Bali ninyi mmemvunjia heshima maskini. Je! matajiri hawawaonei ninyi na kuwavuta mbele ya viti vya hukumu?


Tufuate:

Matangazo


Matangazo