Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 16:12 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

12 Siku ya pili tukafika Neapoli na kutoka hapo tukafika Filippi, mji wa Makedonia, mji ulio mkuu katika wilaya ile, nayo ni Kolonia ya Kirumi; tukawa katika mji huu, tukikaa siku kadha wa kadha.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

12 Kutoka huko, tulikwenda mpaka Filipi, mji wa wilaya ya kwanza ya Makedonia, na ambao pia ni koloni la Waroma. Tulikaa katika mji huo siku kadhaa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

12 Kutoka huko, tulikwenda mpaka Filipi, mji wa wilaya ya kwanza ya Makedonia, na ambao pia ni koloni la Waroma. Tulikaa katika mji huo siku kadhaa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

12 Kutoka huko, tulikwenda mpaka Filipi, mji wa wilaya ya kwanza ya Makedonia, na ambao pia ni koloni la Waroma. Tulikaa katika mji huo siku kadhaa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

12 Kutoka huko tukasafiri hadi Filipi, mji mkuu wa jimbo hilo la Makedonia, uliokuwa koloni ya Warumi. Nasi tukakaa huko siku kadhaa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

12 Kutoka huko tukasafiri hadi Filipi, mji mkuu wa jimbo hilo la Makedonia, uliokuwa koloni ya Warumi. Nasi tukakaa huko siku kadhaa.

Tazama sura Nakili




Matendo 16:12
14 Marejeleo ya Msalaba  

Bassi alipokwisha kuona yale maono, marra tukataka kutoka kwenda Makedonia, kwa kuwa tuliona hakika ya kwamba Bwana ametuita tuwakhubiri Injili.


Tena wanatangaza khabari ya desturi zisizo halali kwetu tuzipokee wala kuzifuata, kwa kuwa sisi tu Warumi.


Paolo akatokewa na maono usiku; alimwona mtu wa Makedonia amesimama, akimsihi akimwambia, Vuka uje Makedonia utusaidie.


Hatta Sila na Timotheo walipotelemka kutoka Makedonia, Paolo akashurutishwa rohoni mwake, akiwashuhudia Wayahudi ya kwamba Yesu ni Kristo.


Mambo hayo yalipokwisha kumalizika, Paolo akaazimu rohoni mwake kupita kati ya Makedonia na Akaia aende Yerusalemi, akisema, Baada ya kuwako huko, yanipasa kuuona na Rumi.


Mji wote ukajaa ghasia, wakaenda mbio wakaingia theatro kwa moyo mmoja, wakiisha kuwakamata Gaio na Aristarko, watu wa Makedonia waliosafiri pamoja na Paolo.


KISHINDO kile kilipokoma, Paolo akawaita wanafunzi akaagana nao, akaondoka aende zake hatta Makedonia.


Alipokwisha kukaa huko miezi mitatu, Wayahudi wakamfanyyia vitimbi, alipotaka kwenda Sham kwa njia ya bahari: bassi akaazimu kurejea kwa ujia ya Makedonia.


Sisi tukatweka baada ya siku ya mikate isiyotiwa chachu, tukatoka Filippi, tukawafikia Troa, safari ya siku tano, tukakaa huko siku saba.


Tukapanda katika merikebu ya Adramuttio iliyokuwa tayari kusafiri hatta miji ya pwani za Asia, tukatweka; Aristarko, Mmakedoni wa Thessalonika, akiwa pamoja nasi.


maana imewapendeza watu wa Makedonia na Akaya kufanya changizo kwa ajili ya watakatifu katika Yerusalemi walio maskini.


PAOLO na Timotheo, watumwa wa Yesu Kristo, kwa watakatifu wote katika Kristo Yesu, walio katika Filipi, pamoja na maaskofu na wakhudumu;


kwa sababu ya ushirika wenu katika kuieneza Injili, tangu siku ya kwanza hatta leo hivi;


bali tukiisha kuteswa kwanza na kutendwa jeuri, kama mjuavyo, katika Filippi, twalithubutu katika Mungu kuinena Injili ya Mungu kwenu, kwa kuishindania sana.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo