Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 15:5 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

5 Lakini baadhi ya madhehebu ya Mafarisayo walioamini wakasimama wakisema, Ni lazima kuwatahiri na kuwaagiza kuishika Torati ya Musa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 Lakini waumini wengine waliokuwa wa kikundi cha Mafarisayo walisimama, wakasema, “Ni lazima watu wa mataifa mengine watahiriwe na kufundishwa kuifuata sheria.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

5 Lakini waumini wengine waliokuwa wa kikundi cha Mafarisayo walisimama, wakasema, “Ni lazima watu wa mataifa mengine watahiriwe na kufundishwa kuifuata sheria.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 Lakini waumini wengine waliokuwa wa kikundi cha Mafarisayo walisimama, wakasema, “Ni lazima watu wa mataifa mengine watahiriwe na kufundishwa kuifuata sheria.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 Ndipo baadhi ya waumini waliokuwa wa dhehebu la Mafarisayo wakasimama na kusema, “Hao watu wa Mataifa lazima watahiriwe na waagizwe kutii Torati ya Musa.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 Ndipo baadhi ya walioamini wa madhehebu ya Mafarisayo wakasimama na kusema, “Hao watu wa Mataifa lazima watahiriwe na waagizwe kutii Torati ya Musa.”

Tazama sura Nakili




Matendo 15:5
14 Marejeleo ya Msalaba  

Hatta akiona wengi miongoni mwa Mafarisayo na Masadukayo wakiujia ubatizo wake, akawaambia, Uzao wa nyoka, nani aliyewaonya mkimbie ghadhabu ijayo?


WAKASHUKA wafu waliotoka Yahudi wakawafundisha ndugu ya kama, Msipotahiriwa na kuifuata desturi ya Musa hamwezi kuokoka.


Kwa kuwa tumesikia ya kwamba watu waliotoka kwetu wamewasumbueni kwa maneno yao, wakipotosha roho zenu, wakisema, ya kuwa hamna buddi kutahiriwa na kuishika Torati, ambao sisi hatukuwapa agizo lo lote;


Nao waliposikia wakamhimidi Mungu, wakamwambia, Ndugu yetu, unaona kwamba Wayahudi walioamini walivyo elfu nyingi, nao wote wana wivu sana kwa ajili ya torati.


Illa neno hili naliungama kwako ya kwamba kwa Njia ile ambayo waiita uzushi, ndivyo ninavyomwabudu Mungu wa baba zetu, nikiyaamini yote yanayopatana na torati na yaliyoandikwa katika vyuo vya manabii.


Kwa maana tamemwona mtu huyu mkorofi, muanzishaji wa fitina katika Mayahudi waliomo duniani, tena ni kichwa cha uzushi wa Wanazorayo.


Lakini tunataka kusikia kwako uonavyo wewe; kwa maana katika khabari za madhehebu hiyo tumekwisha kujua kwamba inanenwa vibaya kilia mahali.


Akaondoka kuhani mkuu na wote waliokuwa pamoja nae (hao ndio walio wa madhehehu ya Masadukayo) wamejaa wivu,


Mtu fullani ameitwa nae amekwisha kutahiriwa? asijifanye kana kwamba hakutabiriwa. Mtu fullani amekwitwa nae hajatahiriwa bado? bassi asitahiriwe.


Lakini Petro alipokuja Antiokia, nalishindana nae uso kwa uso, kwa sababu amepasiwa hukumu;


Lakini, nilipoona ya kuwa njia yao haikwenda sawa sawa na kweli ya Injili, nalimwambia Kefa mbele ya watu wote, Ikiwa wewe uliye Myahudi wafuata desturi za mataifa, wala si za Wayahudi, kwa nini unawashurutisha mataifa kufuata desturi za Wayahudi?


Tufuate:

Matangazo


Matangazo