Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 15:40 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

40 Paolo akamchagua Sila akaondoka, akiombewa na wale ndugu, apewe neema ya Mungu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

40 Naye Paulo akamchagua Sila, na baada ya ndugu wa mahali hapo kumweka chini ya ulinzi wa neema ya Bwana, akaondoka.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

40 Naye Paulo akamchagua Sila, na baada ya ndugu wa mahali hapo kumweka chini ya ulinzi wa neema ya Bwana, akaondoka.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

40 Naye Paulo akamchagua Sila, na baada ya ndugu wa mahali hapo kumweka chini ya ulinzi wa neema ya Bwana, akaondoka.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

40 Lakini Paulo akamchagua Sila na akaondoka baada ya ndugu kuwatakia neema ya Bwana Isa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

40 Lakini Paulo akamchagua Sila na akaondoka baada ya ndugu kuwatakia neema ya Bwana Isa.

Tazama sura Nakili




Matendo 15:40
14 Marejeleo ya Msalaba  

Nae, alipokwisha kufika na kuiona neema ya Mungu akafurahi, akawasihi wote waambatane na Bwana kwa kusudi la moyo.


Ndipo, wakiisha kuomba na kufunga, wakaweka mikono yao juu yao, wakawaacha waende zao.


Na kutoka huko wakasafiri baharini kwenda Antiokia. Huko ndiko walikoombewa neema ya Mungu kwa ile kazi waliyokwisha kuitimiza.


Bassi ikawapendeza mitume na wazee na Kanisa lote kuwachagua watu miongoni mwao na kuwapeleka Antiokia pamoja na Paolo na Barnaba: nao ni hawa, Yuda aliyekwitwa Barsaba, na Sila, watu wakuu katika ndugu.


Tena Yuda na Sila, kwa kuwa wao wenyewe ni manabii, wakawausia ndugu kwa maneno mengi, wakawathubutisha.


Bassi bwana zake walipoona ya kuwa tumaini la faida yao limewapotea, wakawakamata Paolo na Sila, wakawakokota hatta sokoni mbele ya wakuu wa mji;


Wengine wakaamini, wakasuhubiana na Paolo na Sila; na Wayunani waliomcha Mungu, wengi sana, na wanawake wenye eheo si wachache.


Bassi, sasa ndugu, nawawekeni katika mikono ya Mungu, na kwa neno la neema yake, kwake yeye awezae kuwajengeni na kuwapeni urithi pamoja nao wote waliotakasika.


Lakini kwa neema ya Mungu nimekuwa nilivyo; na neema yake iliyo kwangu ilikuwa si burre, bali nalizidi sana kushika kazi kupita wao wote; wala si mimi, bali neema ya Mungu pamoja nami.


Neema ya Bwana Yesu Kristo, na pendo la Mungu, na ushirika wa Roho Mtakatifu ukae nanyi nyote. Amin.


Bwana Yesu Kristo awe pamoja na roho yako. Neema na iwe nanyi. Amin.


Watu wote walio pamoja nami wakusalimu. Tusalimie wale watupendao katika Imani. Neema na iwe nanyi nyote. Amin.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo