Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 15:3 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

3 Bassi, wakisafirishwa na Kanisa, wakapita kati ya inchi ya Foiniki na Samaria, wakitangaza khabari za kuongoka kwao Mataifa; wakawafurahisha ndugu sana.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 Basi, kanisa liliwaaga, nao walipokuwa wanapitia Foinike na Samaria waliwaeleza watu jinsi mataifa mengine yalivyomgeukia Mungu. Habari hizo zikawafurahisha sana ndugu hao wote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

3 Basi, kanisa liliwaaga, nao walipokuwa wanapitia Foinike na Samaria waliwaeleza watu jinsi mataifa mengine yalivyomgeukia Mungu. Habari hizo zikawafurahisha sana ndugu hao wote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 Basi, kanisa liliwaaga, nao walipokuwa wanapitia Foinike na Samaria waliwaeleza watu jinsi mataifa mengine yalivyomgeukia Mungu. Habari hizo zikawafurahisha sana ndugu hao wote.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 Hivyo wakatumwa na waumini. Wakapitia Foinike na Samaria, wakielezea jinsi watu wa Mataifa walivyoongoka. Habari hizi zikaleta furaha kubwa kwa ndugu wote.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

3 Hivyo wakasafirishwa na waumini. Wakiwa njiani wakapitia nchi ya Foinike na Samaria, wakawaeleza jinsi watu wa Mataifa walivyookoka. Habari hizi zikaleta furaha kubwa kwa ndugu wote.

Tazama sura Nakili




Matendo 15:3
27 Marejeleo ya Msalaba  

Tena kufanya furaha na kuona furaha kulikuwa wajib, kwa maana huyu ndugu yako alikuwa amekufa, nae amefufuka: alikuwa amepotea, nae ameonekana.


Siku zile akasimama Petro kati ya wanafunzi, akasema (jumla ya majina ilipata mia na ishirini),


Mataifa waliposikia hayo wakafurahi, wakalitukuza neno la Bwana, nao waliokuwa wamekusudiwa uzima wa milele wakaamini.


Na wanafunzi walijaa furaha na Roho Mtakatifu.


Hatta walipolika wakalikutanisha Kanisa, wakawaeleza mambo yote aliyoyafanya Mungu pamoja nao, na ya kwaruba amewafungulia mataifa mlango wa imani.


WAKASHUKA wafu waliotoka Yahudi wakawafundisha ndugu ya kama, Msipotahiriwa na kuifuata desturi ya Musa hamwezi kuokoka.


Bassi mkutano wote wakanyamaza, wakawasikiliza Barnaba na Paolo wakiwapasha khabari za ishara na maajabu ambayo Mungu aliyafanya kwa ujumbe wao katika mataifa.


Bassi ikawapendeza mitume na wazee na Kanisa lote kuwachagua watu miongoni mwao na kuwapeleka Antiokia pamoja na Paolo na Barnaba: nao ni hawa, Yuda aliyekwitwa Barsaba, na Sila, watu wakuu katika ndugu.


Tena Yuda na Sila, kwa kuwa wao wenyewe ni manabii, wakawausia ndugu kwa maneno mengi, wakawathubutisha.


Walipofika Yerusalemi wakakaribishwa na Kanisa na mitume na wazee, nao wakawaeleza mambo yote Mungu aliyoyafanya pamoja nao.


Nao walimsindikiza Paolo wakampeleka hatta Athene; na wakiisha kupokea maagizo kuwapelekea Sila na Timotheo, ya kama wasikawie kumfuata, wakaenda zao.


wakihuzunika zaidi kwa sababu ya neno lile alilosema, ya kwamba hawatamtazama uso tena. Wakamsindikiza hatta merikebuni.


Hatta tulipotimiza siku zile tukaondoka tukaenda zetu, na watu wote pamoja na wake zao na watoto wao wakatusindikiza hatta nje ya mji, wakapiga magoti pwani wakaomba:


Na kutoka huko ndugu, waliposikia khabari zetu, wakaja kutulaki mpaka Appiiforo na Trestaberne. Paolo alipowaona akamshukuru Mungu, akachangaʼmka.


Na mitume walioko Yerusalemi, waliposikia ya kwamba Samaria imelikubali neno la Mungu, wakawapelekea Petro na Yohana.


wakati wo wote nitakaosafiri kwenda Hispania nitakuja kwenu, kwa maana nataraja kuwaona ninyi katika kusafiri kwangu, na kupelekwa mbele nanyi, moyo wangu ushibe kwenu ijapokuwa ni kidogo.


bassi mtu aliye yote asimdharau, lakini msafirisheni kwa amani, illi aje kwangu; maana ninamtazamia pamoja na ndugu zetu.


Labda nitakaa kwenu; naam, labda nitashinda kwenu wakati wa baridi, mpate kunisafirisha wakati uwao wote nitakapokwenda.


na kupita kwenu na kuendelea hatta Umakedoni; na tena toka Makedonia kurudi kwenu na kusafirishwa nanyi kwenda Yahudi.


Zena, mjua sharia, na Apollo uwusafirishe kwa bidii; wasipungukiwe cho chote.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo