Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Matendo 15:29 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

29 mjiepushe na vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na damu, na nyama zilizosongwa, na asharati. Mkijizuia na hayo, mtafanya vema. Salamu.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

29 Msile vyakula vilivyotambikiwa vinyago; msinywe damu; msile nyama ya mnyama aliyenyongwa; na mjiepushe na uasherati. Mtakuwa mmefanya vema kama mkiepa kufanya mambo hayo. Wasalaam!”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

29 Msile vyakula vilivyotambikiwa vinyago; msinywe damu; msile nyama ya mnyama aliyenyongwa; na mjiepushe na uasherati. Mtakuwa mmefanya vema kama mkiepa kufanya mambo hayo. Wasalaam!”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

29 Msile vyakula vilivyotambikiwa vinyago; msinywe damu; msile nyama ya mnyama aliyenyongwa; na mjiepushe na uasherati. Mtakuwa mmefanya vema kama mkiepa kufanya mambo hayo. Wasalaam!”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

29 Kwamba mjiepushe na vyakula vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na damu, au kula nyama ya mnyama aliyenyongwa, na mjiepushe na uasherati. Mkiyaepuka mambo haya, mtakuwa mmefanya vyema. Kwaherini.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

29 Kwamba mjiepushe na vyakula vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na damu, au kula nyama ya mnyama aliyenyongwa, na mjiepushe na uasherati. Mkiyaepuka mambo haya, mtakuwa mmefanya vyema. Kwaherini.

Tazama sura Nakili

Matendo 15:29
20 Marejeleo ya Msalaba  

Na mwingine nae akasema, Nitakufuata, Bwana, lakini kwanza nipe rukhusa nikawaage watu wa nyumbani mwangu.

balituwaandikie wajiepushe na unajisi wa sanamu na asharati na nyama zilizosongwa na damu.

bali aliagana nao, akisema. Sina buddi kufanya siku kuu hii inayokuja Yerusalemi: lakini nitarejea kwenu, Mungu akinijalia.

Kwa khabari za watu wa mataifa walioamini, tumekwisha kutoa hukumu yetu, wsio wasishike neno linginelo illa kujilinda nafsi zao na vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na damu, na kitu kilichosongwa, na uasharati.

Hatta nilipopewa khabari kwamba patakuwa na vitimbi juu ya mtu huyu, marra nikampeleka kwako, nikawaagiza na wale walioshitaki, wanene khabari zake mbele yako. Salamu.

Nami nilipokuwa pamoja nanyi na kuhitaji sikumlemea mtu. Maana ndugu walipokuja kutoka Makedonia walinipa kadiri ya mahitaji yangu; na katika mambo yote nalijilinda nafsi yangu nisiwalemee hatta kidogo; tena nitajilinda.

Khatimae, ndugu, kwa kherini; mtimilike, mfarajike, nieni mamoja, mkae katika imani; na Mungu wa upendo na amani awe pamoja nanyi.

Usimwekee mtu mikono kwa haraka, wala usishiriki dhambi za watu wengine.

Dini iliyo safi na isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni hii, Kwenda kuwatazama yatima na wajane katika shidda yao, na kujilinda pasipo mawaa katika dunia.

Watoto wangu wadogo, jilindeni nafsi zenu na sanamu.

Kwake Yeye awezae kuwalinda ninyi msijikwae, na kuwasimamisha mbele ya utukufu wake bila mawaa katika furaha kuu,

Lakini ninayo maneno machache juu yako, kwa kuwa unao huko watu washikao mafundisho ya Balaam, yeye aliyemfundisha Balak atie ukwazo mbele ya wana wa Israeli, wavile vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na kuzini.

Lakini nina maneno machache juu yako, ya kwamba wamwacha yule mwanamke Yezebel, yeye ajiitae nabii, nae awafundisha watumishi wangu na kuwapoteza, illi wazini na kula vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo