Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 15:28 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

28 Kwa maana ilimpendeza Roho Mtakatifu na sisi, tusiwatwike mzigo illa hayo yaliyo faradhi,

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

28 Basi, Roho Mtakatifu na sisi tumekubali tusiwatwike mzigo zaidi ya mambo haya muhimu:

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

28 Basi, Roho Mtakatifu na sisi tumekubali tusiwatwike mzigo zaidi ya mambo haya muhimu:

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

28 Basi, Roho Mtakatifu na sisi tumekubali tusiwatwike mzigo zaidi ya mambo haya muhimu:

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

28 Kwa maana imempendeza Roho wa Mungu na sisi tusiwatwike mzigo wowote mkubwa zaidi ya mambo haya yafuatayo ambayo ni ya lazima:

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

28 Kwa maana imempendeza Roho wa Mwenyezi Mungu na sisi tusiwatwike mzigo wowote mkubwa zaidi ya mambo haya yafuatayo ambayo ni ya lazima:

Tazama sura Nakili




Matendo 15:28
14 Marejeleo ya Msalaba  

kwa maana nira yangu laini, na mzigo wangu mwepesi.


Kwa maana hufunga mizigo mizito isiyochukulika na kuwatwika watu mabegani mwao; wasitake wenyewe kuisogeza kwa kidole chao.


Lakini ajapo yeye, Roho ya kweli, atawaongozeni katika yote iliyo kweli: kwa maana hatasema kwa shauri lake yeye, lakini yote atakayosikia, atayasema, na mambo yajayo atawapasha khabari yake.


Kwa sababu hiyo mimi naamua hivi: Tusiwataabishe wale waliomgeukia Mungu katika Mataifa:


bassi tumeona vema tukiwa tumepatana kwa moyo mmoja, kuwachagua watu na kuwapeleka kwenu pamoja na wapendwa wetu Barnaba na Paolo,


Na Mungu, ajuae mioyo ya watu, akawashuhudia, akiwapa Roho Mtakatifu vilevile kama alivyotupa sisi;


Bassi walipokuwa wakipita kati ya miji ile, wakawapa zile amri zilizoamriwa na mitume na wazee walioko Yerusalemi, illi wazishike.


Na sisi tu mashahidi wa mambo haya, pamoja na Roho Mtakatifu ambae Mungu amewapa wote wamtiio.


Mtu akijiona kuwa nabii au mtu wa rohoni, na ayatambue haya ninayowaandikieni, ya kwamba ni maagizo ya Bwana.


Kwa khabari za mabikira sina amri ya Bwana, lakini natoa shauri langu, mimi niliyejaliwa kuwa mwaminifu kwa rehema za Bwana.


Lakini yu kheri zaidi akikaa kama alivyo; ndivyo nionavyo mimi; nami nadhani ya kuwa mimi nami nina Roho ya Bwana.


Bassi yeye anaekataa, hakatai mwana Adamu bali Mungu, anaewapeni Roho yake Mtakatifu.


Waliofunuliwa ya kuwa si kwa ajili yao wenyewe, bali kwa ajili yetu walitumika katika mambo hayo, ambayo sasa yamekhubiriwa kwenu na wale waliowakhubiri ninyi Injili kwa Roho Mtakatifu aliyetumwa kutoka mbinguni. Mambo hiayo malaika wanatamani kuyachuugulia.


Lakini nawaambia ninyi, nao wengine walio katika Thuatera, wo wote wasio na mafundisho haya, wasiozijua fumbo za Shetani kama vile wasemavyo, Sitaweka juu yen umzigo mwungine.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo