Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 15:23 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

23 Wakaandika hivi kwa mikono yao, Mitume na wazee na ndugu, kwa ndugu zetu walioko Antiokia na Shami na Kilikia, walio wa mataifa, salamu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

23 Wakawapa barua hii: “Sisi mitume na wazee, ndugu zenu, tunawasalimuni nyinyi ndugu wa mataifa mengine mlioko huko Antiokia, Siria na Kilikia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

23 Wakawapa barua hii: “Sisi mitume na wazee, ndugu zenu, tunawasalimuni nyinyi ndugu wa mataifa mengine mlioko huko Antiokia, Siria na Kilikia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

23 Wakawapa barua hii: “Sisi mitume na wazee, ndugu zenu, tunawasalimuni nyinyi ndugu wa mataifa mengine mlioko huko Antiokia, Siria na Kilikia.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

23 Wakatumwa na barua ifuatayo: Sisi mitume na wazee, ndugu zenu. Kwa waumini wa Mataifa mlio Antiokia, Siria na Kilikia. Salamu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

23 Wakatumwa na barua ifuatayo: Sisi mitume na wazee, ndugu zenu, Kwa ndugu Mataifa mlioamini mlioko Antiokia, Shamu na Kilikia: Salamu.

Tazama sura Nakili




Matendo 15:23
21 Marejeleo ya Msalaba  

Khabari zake zikaenea katika Sham yote; wakamletea watu waliokuwa hawawezi, walioshikwa mi maradhi mbali mbali na mateso, nao wenye pepo, na wenye kifafa, na wenye kupooza; akawaponya.


Waliposikia maneno haya wakanyamaza, wakamtukuza Mungu, wakisema, Bassi, Mungu amewajalia mataifa nao toba liletalo uzima.


Baadhi ya hao walikuwa watu wa Kupro na Kurene, nao walipofika Antiokia wakasema na Wahelenisti, wakakhubiri khabari njema za Bwana Yesu.


Hatta walipolika wakalikutanisha Kanisa, wakawaeleza mambo yote aliyoyafanya Mungu pamoja nao, na ya kwaruba amewafungulia mataifa mlango wa imani.


WAKASHUKA wafu waliotoka Yahudi wakawafundisha ndugu ya kama, Msipotahiriwa na kuifuata desturi ya Musa hamwezi kuokoka.


Bassi baada ya Paolo na Barnaba kushindana na watu hawa na kuhujiana nao sana, ndugu wakaamuru kwamba Paolo na Barnaba na wengine miongoni mwao wapande kwenda Yerusalemi kwa mitume na wazee kwa khabari ya swali hilo.


Bassi ikawapendeza mitume na wazee na Kanisa lote kuwachagua watu miongoni mwao na kuwapeleka Antiokia pamoja na Paolo na Barnaba: nao ni hawa, Yuda aliyekwitwa Barsaba, na Sila, watu wakuu katika ndugu.


Walipofika Yerusalemi wakakaribishwa na Kanisa na mitume na wazee, nao wakawaeleza mambo yote Mungu aliyoyafanya pamoja nao.


Akapita katika Shami na Kilikia akawatia moyo makanisa.


Paolo akazidi kukaa huko siku nyingi, kiisha akaagana na ndugu akatweka kwenda Shami; na Priskilla na Akula wakaenda pamoja nae, alipokwisha kunyoa kichwa chake katika Kenkrea; maana alikuwa ana nadhiri.


Kwa khabari za watu wa mataifa walioamini, tumekwisha kutoa hukumu yetu, wsio wasishike neno linginelo illa kujilinda nafsi zao na vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na damu, na kitu kilichosongwa, na uasharati.


Na tulipoona Kupro tukaiacha upande wa kushoto: tukasafiri hatta Shami tukashuka Turo. Kwa maana huko ndiko marikebu yetu itakakoshusha shehena yake.


Klaudio Lusia kwa liwali il aziz Feliki salamu!


Lakini baadhi ya watu wa sunagogi lililokwitwa sunagogi la Malibertino, na la Wakurene na la Waiskanderia, na la wale wa Kilikia na Asia, wakaondoka wakajadiliana na Stefano:


Khalafu nalikwenda pande za Sham na Kilikia.


YAKOBO, mtumwa wa Mungu, na Bwana Yesu Kristo, kwa kabila thenashara zilizotawanyika, salamu,


Mtu akija kwenu, nae haleti mafundisho hayo, msimkaribishe nyumbani mwenu, wala msimpe salamu.


Wa-toto wa ndugu yako aliye mteule, wakusalimu.


Neema, na rehema, na amani zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Bwana wetu Yesu Kristo zitakuwa pamoja nasi katika kweli na upendo.


Lakini nataraja kukuona karibu na kusema nawe mdomo kwa mdonm.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo