Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 15:1 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 WAKASHUKA wafu waliotoka Yahudi wakawafundisha ndugu ya kama, Msipotahiriwa na kuifuata desturi ya Musa hamwezi kuokoka.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Basi, watu wengine walifika Antiokia kutoka Yudea wakaanza kuwafundisha wale ndugu wakisema, “Kama hamtatahiriwa kufuatana na mapokeo kama alivyoamuru Mose, hamtaweza kuokolewa.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Basi, watu wengine walifika Antiokia kutoka Yudea wakaanza kuwafundisha wale ndugu wakisema, “Kama hamtatahiriwa kufuatana na mapokeo kama alivyoamuru Mose, hamtaweza kuokolewa.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Basi, watu wengine walifika Antiokia kutoka Yudea wakaanza kuwafundisha wale ndugu wakisema, “Kama hamtatahiriwa kufuatana na mapokeo kama alivyoamuru Mose, hamtaweza kuokolewa.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Baadhi ya watu wakashuka Antiokia kutoka Yudea, nao wakawa wanawafundisha waumini: “Msipotahiriwa kulingana na desturi aliyofundisha Musa, hamwezi kuokoka.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Baadhi ya watu wakashuka Antiokia kutoka Uyahudi, nao wakawa wanawafundisha wandugu: “Msipotahiriwa kufuatana na desturi aliyofundisha Musa, hamwezi kuokoka.”

Tazama sura Nakili




Matendo 15:1
25 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa sababu hii Musa aliwapa tohara, si kwamba yatoka kwa Musa bali kwa babu zenu: nanyi siku ya sabato humtahiri mtu.


Siku zile akasimama Petro kati ya wanafunzi, akasema (jumla ya majina ilipata mia na ishirini),


Bassi ikawapendeza mitume na wazee na Kanisa lote kuwachagua watu miongoni mwao na kuwapeleka Antiokia pamoja na Paolo na Barnaba: nao ni hawa, Yuda aliyekwitwa Barsaba, na Sila, watu wakuu katika ndugu.


Wakaandika hivi kwa mikono yao, Mitume na wazee na ndugu, kwa ndugu zetu walioko Antiokia na Shami na Kilikia, walio wa mataifa, salamu.


Kwa kuwa tumesikia ya kwamba watu waliotoka kwetu wamewasumbueni kwa maneno yao, wakipotosha roho zenu, wakisema, ya kuwa hamna buddi kutahiriwa na kuishika Torati, ambao sisi hatukuwapa agizo lo lote;


Bassi, wakisafirishwa na Kanisa, wakapita kati ya inchi ya Foiniki na Samaria, wakitangaza khabari za kuongoka kwao Mataifa; wakawafurahisha ndugu sana.


Tena Yuda na Sila, kwa kuwa wao wenyewe ni manabii, wakawausia ndugu kwa maneno mengi, wakawathubutisha.


Lakini baadhi ya madhehebu ya Mafarisayo walioamini wakasimama wakisema, Ni lazima kuwatahiri na kuwaagiza kuishika Torati ya Musa.


Nao waliposikia wakamhimidi Mungu, wakamwambia, Ndugu yetu, unaona kwamba Wayahudi walioamini walivyo elfu nyingi, nao wote wana wivu sana kwa ajili ya torati.


maana tumemsikia akisema kwamba Yesu huyo Mnazareti atapaharibu pahali hapa, na kuzihadili desturi tulizopewa na Musa.


KIISHA, baada va miaka kumi na minane, nalipanda kwenda Yerusalemi pamoja na Barnaba, nikamchukua na Tito pamoja nami.


Maana katika Kristo Yesu kutahiriwa hakufai neno wala kutokutahiriwa, bali imani itendayo kazi kwa upendo.


Wote watakao kuonekana ni wazuri kwa mwili, ndio wanaokushurutisheni kutahiriwa: wasiudhiwe tu kwa ajili ya msalaba wa Kristo.


Bassi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au viuvwaji au kwa sababu ya siku kuu au mwandamo wa mwezi, au sabato;


Angalieni intu asiwateke kwa filosofia yake na madanganya matupu, kwa jinsi ya mapokeo ya wana Adamu, kwa jinsi ya mafundisho ya awali ya ulimwengu, wala si kwa jinsi ya Kristo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo