Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 14:23 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

23 Na walipokwisha kuchagua wazee katika killa mji, na kuomba pamoja na kufunga, wakawaweka kafika mikono ya Bwana waliyemwamini.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

23 Waliteua wazee katika kila kanisa kwa ajili ya waumini, kisha, kwa kusali na kufunga, wakawaweka chini ya ulinzi wa Bwana ambaye walikuwa wanamwamini.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

23 Waliteua wazee katika kila kanisa kwa ajili ya waumini, kisha, kwa kusali na kufunga, wakawaweka chini ya ulinzi wa Bwana ambaye walikuwa wanamwamini.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

23 Waliteua wazee katika kila kanisa kwa ajili ya waumini, kisha, kwa kusali na kufunga, wakawaweka chini ya ulinzi wa Bwana ambaye walikuwa wanamwamini.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

23 Nao baada ya kuwateua wazee katika kila kundi la waumini wa Isa, kwa kufunga na kuomba wakawakabidhi kwa Bwana Isa waliyemwamini.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

23 Nao baada ya kuwateua wazee katika kila kundi la waumini, kwa kufunga na kuomba wakawakabidhi kwa Bwana Isa waliyemwamini.

Tazama sura Nakili




Matendo 14:23
28 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini namna hii haitoki illa kwa kusali na kufunga.


Akaweka thenashara, wapate kuwa pamoja nae, na kusudi awatume kukhubiri,


nae mjane wa miaka themanini na mine; asiyeondoka hekaluni, kwa kufunga na kusali akiabudu usiku na mchana.


Yesu akalia kwa sauti kuu, akasema, Baba, mikononi mwako naiweka roho yangu: na alipokwisha kusema haya akatoa roho.


akianza tangu ubatizo wa Yohana, hatta siku ile alipochukuliwa kwetu kwenda juu, lazima mmoja wao afanywe shahidi wa kufufuka kwake pamoja nasi.


Wakasali, wakasema, Wewe, Bwana, ujuae mioyo ya watu wote, tuonyeshe ni nani uliyemchagua katika hawa wawili,


Wakafanya hivyo, wakawapelekea wazee kwa mikono ya Barnaha na Saul.


Na kutoka huko wakasafiri baharini kwenda Antiokia. Huko ndiko walikoombewa neema ya Mungu kwa ile kazi waliyokwisha kuitimiza.


Wakaandika hivi kwa mikono yao, Mitume na wazee na ndugu, kwa ndugu zetu walioko Antiokia na Shami na Kilikia, walio wa mataifa, salamu.


Walipofika Yerusalemi wakakaribishwa na Kanisa na mitume na wazee, nao wakawaeleza mambo yote Mungu aliyoyafanya pamoja nao.


Mitume na wazee wakakusanyika wapate kulifikiri neno hilo.


Toka Mileto Faolo akatuma watu kwenda hatta Efeso, akawaita wazee wa Kanisa.


Bassi, sasa ndugu, nawawekeni katika mikono ya Mungu, na kwa neno la neema yake, kwake yeye awezae kuwajengeni na kuwapeni urithi pamoja nao wote waliotakasika.


Wala si hivyo tu, bali alichaguliwa na makanisa asafiri pamoja nias katika jambo la neema hii inayokhudumiwa nasi, illi Bwana atukuzwe, ikadhihirike ya kuwa mioyo yenu ilikuwa tayari.


USIMKEMEE mzee, bali mwonye kama baba, na wadogo wako kama ndugu:


Usimwekee mtu mikono kwa haraka, wala usishiriki dhambi za watu wengine.


Kwa sababu hiyo nimepata mateso haya, wala sitahayariki: maana namjua yeye niliyemwamini, na kusadiki kwamba aweza kukilinda kile nilichakiweka amana kwake hatta siku ile.


Na yale uliyoyasikia kwangu kwa mashahidi wengi, uwakabidbi hayo watu waaminifu watakaofaa kuwafundisha na wengine.


Kwa sababu hii nalikuaeba katika Krete, illi nyatengeneze yaliyosalia, na kuweka wazee katika killa mji kama nilivyokuamuru;


Mtu wa kwenu amekuwa hawezi? na awaite wazee wa kanisa wakamwombee, wakimpaka mafuta kwa jina la Bwana.


NAWASIHI wazee walio kwenu, mimi niliye mzee, mwenzi wao, na shahidi wa mateso ya Kristo, na mshirika wa utukufu utakaofunuliwa baadae;


Na Mungu wa neema yote, aliyewaita kuingia utukufu wake wa milele katika Kristo, mkiisha kuteswa kwa muda kidogo, yeye mwenyewe atawatengeneza, atawathubutisha, atawatia nguvu.


MZEE kwa bibi mteule na watoto wake niwapendao katika kweli; wala si mimi peke yangu, bali na ndugu wote waijuao ile kweli;


MZEE kwa Gaio mpenzi, nimpendae katika kweli.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo