Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 14:15 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

15 Sisi nasi tu wana Adamu hali moja na ninyi; twawakhubiri khabari njema mgenke na kuyaacha mambo haya ya ubatili na kumwelekea Mungu aliye hayi, aliyeumba mbingu na inchi na bahari na vitu vyotc vilivyomo:

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

15 “Ndugu, kwa nini mnafanya mambo hayo? Sisi pia ni binadamu kama nyinyi. Na, tuko hapa kuwahubirieni Habari Njema, mpate kuziacha hizi sanamu tupu, mkamgeukie Mungu aliye hai, Mungu aliyeumba mbingu na dunia, bahari na vyote vilivyomo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

15 “Ndugu, kwa nini mnafanya mambo hayo? Sisi pia ni binadamu kama nyinyi. Na, tuko hapa kuwahubirieni Habari Njema, mpate kuziacha hizi sanamu tupu, mkamgeukie Mungu aliye hai, Mungu aliyeumba mbingu na dunia, bahari na vyote vilivyomo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

15 “Ndugu, kwa nini mnafanya mambo hayo? Sisi pia ni binadamu kama nyinyi. Na, tuko hapa kuwahubirieni Habari Njema, mpate kuziacha hizi sanamu tupu, mkamgeukie Mungu aliye hai, Mungu aliyeumba mbingu na dunia, bahari na vyote vilivyomo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

15 “Enyi watu, kwa nini mnafanya mambo haya? Sisi ni wanadamu tu kama ninyi! Tunawaletea Habari Njema, tukiwaambia kwamba mgeuke mtoke katika mambo haya yasiyofaa, mmwelekee Mungu aliye hai, aliyeziumba mbingu na nchi na bahari na vitu vyote vilivyomo.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

15 “Enyi watu, kwa nini mnafanya mambo haya? Sisi ni wanadamu tu kama ninyi! Tunawaletea habari njema, tukiwaambia kwamba mgeuke mtoke katika mambo haya yasiyofaa, mmwelekee Mungu aliye hai, aliyeziumba mbingu na nchi na bahari na vitu vyote vilivyomo.

Tazama sura Nakili




Matendo 14:15
67 Marejeleo ya Msalaba  

Simon Petro akajibu, akasema, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hayi.


Maana kama vile Baba alivyo na uzima nafsini mwake, vivyo hivyo alimpa na Mwana kuwa na uzima nafsini mwake;


Yeye anenae kwa nafsi yake tu, hutafuta utukufu wake mwenyewe; bali yeye anaetafuta utukufu wake aliyempeleka, huyu ni wa kweli wala ndani yake hamna udhalimu.


Petro akamwinua, akasema, Simama, mimi nami ni mwana Adamu.


Na sisi tunawakhubirieni ahadi ile waliyopewa baba zetu, ya kwamba Mungu ametutimizia sisi watoto wao ahadi hiyo, kwa kumfufua Yesu:


Hatta walipokwisha kuikhubiri Injili katika niji ule, na kupata wanafunzi wengi, wakarejea hatta Lustra na Ikonio na Antiokia,


wakakaa huko, wakiikhubiri Injili.


kiisha akawaleta nje akasema, Bwana zangu, nifanye nini nipate kuokoka?


Wanaume, naoua kwamba safari hii itakuwa ina madhara na hasara nyingi, si ya shehena na merikebu tu, illa na ya maisha zetu pia.


Na tulipokuwa tumekaa wakati mwingi bila kula chakula, Paolo akasimama katikati yao, akasema, Wanaume, ingalikuwa kheri kama mngalinisikiliza na kutokungʼoa nanga huko Krete, na kupata madhara haya na hasara hii.


Bassi, wanaume, changaʼmkani; kwa sababu namwamini Mungu, ya kwamba yatakuwa vile vile kama nilivyoambiwa.


Nao waliposikia, wakampaazia Mungu sauti zao kwa moyo mmoja, wakisema, Mola, wewe ndiwe Mungu, ndiwe uliyefanya mbingu na inchi na bahari na vitu vyote vilivyomo:


Siku ya pili yake akawatokea walipokuwa wakishindana, akataka kuwapatanisha, akisema, Enyi bwana zangu, ninyi m ndugu: Mbona mnadhulumiana?


Bassi, kwa khabari ya kuvila vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu; twajua ya kuwa sanamu si kitu katika ulimwengu, na ya kuwa hapana Mungu mwingine illa mmoja tu.


Bassi nasema neno bili, tena nashuhudu katika Bwana, tangu sasa msienende kama Mataifa waendavyo, katika ubatili wa nia zao,


Maana wao wenyewe wanatangaza khabari zetu, jinsi kulivyokuwa kuingia kwetu kwenu; na jinsi mlivyomgeukia Mungu, mkaziacha sanamu illi kumtumikia Mungu aliye hayi, wa kweli,


Lakini nikikawia, upate kujua sana jinsi iwapasavyo watu kuenenda katika nyumba ya Mungu iliyo kanisa la Mungu aliye hayi, nguzo na msingi wa kweli.


Angalieni, ndugu zangu, usiwe katika mmoja wenu moyo mbovu wa kutokuamini, kwa kujitenga na Mungu aliye hayi.


Eliya alikuwa mwana Adamu mwenye tabia moja na sisi, akaomba kwa bidii mvua isinye: na mvua haikunya juu ya inchi muda wa miaka mitatu na miezi sita.


akasema kwa sauti kuu, Mcheni Mungu, kamtukuzeni, maana saa ya hukumu yake imekuja. Kamsujuduni yeye aliyezifanya mbingu na inchi na bahari na chemchemi za maji.


Nikaanguka mbele ya miguu yake, nimsujudie, akaniambia, Angalia, usifanye hivi: mimi mjoli wako na mmoja wa ndugu zako walio na ushuhuda wa Yesu. Msujudu Mungu: kwa maana ushuhuda wa Yesu ni roho ya unabii.


Nikamwonu nyama, na wafalme wa inchi, na majeshi yao, wamekutana kufanya vita na yeye aketiye juu ya farasi yule, na na majeshi yake.


Akaniambia, Angalia, usifanye hivyo; mimi mjoli wako, na wa ndugu zako manabii na wa wale washikao maneno ya kitabu hiki. Msujuduni Mungu.


Umestahili, Bwana, Mungu wetu, kuupokea utukufu na heshima na nweza; kwa kuwa wewe ndiwe uliyeviumba vitu vyote, na kwa sababu ya mapenzi yako vilikuwako, vikaumbwa.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo