Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 13:48 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

48 Mataifa waliposikia hayo wakafurahi, wakalitukuza neno la Bwana, nao waliokuwa wamekusudiwa uzima wa milele wakaamini.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

48 Watu wa mataifa mengine waliposikia jambo hilo walifurahi, wakausifu ujumbe wa Mungu; na wale waliokuwa wamechaguliwa kupata uhai wa milele, wakawa waumini.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

48 Watu wa mataifa mengine waliposikia jambo hilo walifurahi, wakausifu ujumbe wa Mungu; na wale waliokuwa wamechaguliwa kupata uhai wa milele, wakawa waumini.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

48 Watu wa mataifa mengine waliposikia jambo hilo walifurahi, wakausifu ujumbe wa Mungu; na wale waliokuwa wamechaguliwa kupata uhai wa milele, wakawa waumini.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

48 Watu wa Mataifa waliposikia haya wakafurahi na kulitukuza neno la Mwenyezi Mungu; nao wote waliokuwa wamekusudiwa uzima wa milele wakaamini.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

48 Watu wa Mataifa waliposikia haya wakafurahi na kulitukuza neno la Bwana Isa; nao wote waliokuwa wamekusudiwa uzima wa milele wakaamini.

Tazama sura Nakili




Matendo 13:48
31 Marejeleo ya Msalaba  

Na hawo watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele: bali wenye haki katika uzima wa milele.


Na wale wanafunzi edashara wakaenda Galilaya hatta mlima ule aliowaagiza Yesu.


Sababu mimi nami ni mtu aliyewekwa chini ya mamlaka, nina askari chini yangu: nikimwambia huyu, Nenda, huenda: na huyu, Njoo, huja; na mtumishi wangu, Fanya hivi, hufanya.


Na kondoo wengine ninao, wasio wa zizi hili; na hao nao imenipasa kuwaleta, na sauti yangu wataisikia; na kutakuwapo kundi moja na mchunga mmoja.


wala si kwa ajili ya taifa lile tu, lakini pamoja na haya awakusanye watoto wa Mungu waliotawanyika wawe wamoja.


Ndipo yule liwali, alipoyaona yaliyotendeka, akaamini akiyastaajabia mafundisho ya Bwana.


Na walipokuwa wakitoka katika sunagogi la Wayahudi, watu wa mataifa wakawasihi kuwaambia maneno haya sabato ya pili.


Bassi baada ya Paolo na Barnaba kushindana na watu hawa na kuhujiana nao sana, ndugu wakaamuru kwamba Paolo na Barnaba na wengine miongoni mwao wapande kwenda Yerusalemi kwa mitume na wazee kwa khabari ya swali hilo.


Wakausoma, wakafurahi kwa ajili ya faraja ile.


Nao waliolipokea neno lake kwa furaha wakabatizwa: na siku ile wakazidishiwa watu wapata elfu tatu.


wakimsifu Mungu, na kuwapendeza wutu wote. Bwana akalizidisha kanisa killa siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa.


Sisi tukatangulia kwenda merikebuni, tukasafiri hatta Asso, tukikusudia kumpokea Paolo huko: kwa maana ndivyo alivyoagiza, yeye mwenyewe akiazimu kwenda kwa miguu.


Nikasema, Nifanye nini, Bwana? Bwana akaniambia, Simama, uende hatta Dameski, na huko utaambiwa khabari za mambo vote yaliyoamriwa uyafanye.


Wakiislia kuwekana kwa siku, wakaja kwake nyumbani kwake, watu wengi sana, akawaeleza kwa taratibu na kuushuhudia ufalme wa Mungu, akiwaonya mambo yake Yesu, kwa maneno ya sharia ya Musa na ya manabii, tangu assubuhi hatta jioni.


Ikawa furaha kubwa kafika mji ule.


Imekuwaje bassi? Kitu kile ambacho Israeli alikuwa akikitafuta hakukipata, lakini wale waliochaguliwa walikipata, na wengine walitiwa ugumu.


KILLA nafsi itumikie mamlaka makuu; kwa maana hapana mamlaka yasiyotoka kwa Mungu: na mamlaka yaliyopo yameamriwa na Mungu.


Na twajua ya kuwa mambo yote hushiriki kazi moja, ndio kuwapatia mema wale wampendao Mungu, yaani wale walioitwa kwa kusudi lake.


Tena nawasihi, ndugu, (mnaijua nyumba ya Stefano kwamba ni malimbuko ya Akaia, nao wamejitia katika kazi ya kuwakhudumu watakatifu),


ambae ndani yake sisi tumepata urithi, tukichaguliwa tangu awali kwa kusudi lake yeye afanyae yote kwa shauri la nia yake;


na ubora wa ukuu wa uweza wake ndani yetu tuaminio, jinsi ulivyo, kwa kadiri ya kazi ya nguvu zake hodari,


kama alivyotuchagua katika yeye kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, tuwe watakatifu, wasio khatiya mbele zake, katika pendo.


Kwa kuwa ametuchagua tangu zamani illi tufanywe waua wake yeye kwa njia ya Yesu Kristo, kwa mapenzi ya nia yake,


ILIYOBAKI, ndugu, tuombeeni, neno la Bwana liendelee, likatunzwe vilevile kama ilivyo kwenu;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo