Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 13:46 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

46 Paolo na Barnaba wakanena kwa uthabiti wakasema, Ilikuwa lazima neno la Mungu linenwe kwenu kwanza: illakini kwa kuwa mnalisukumia mbali, wala hamjioni nafsi zenu kuwa mmestahili uzima wa milele, angalieni, twawageukia mataifa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

46 Hata hivyo, Paulo na Barnaba waliongea kwa uhodari zaidi, wakasema, “Ilikuwa ni lazima neno la Mungu liwafikieni nyinyi kwanza; lakini kwa kuwa mmelikataa na kujiona hamstahili uhai wa milele, basi, tunawaacheni na kuwaendea watu wa mataifa mengine.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

46 Hata hivyo, Paulo na Barnaba waliongea kwa uhodari zaidi, wakasema, “Ilikuwa ni lazima neno la Mungu liwafikieni nyinyi kwanza; lakini kwa kuwa mmelikataa na kujiona hamstahili uhai wa milele, basi, tunawaacheni na kuwaendea watu wa mataifa mengine.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

46 Hata hivyo, Paulo na Barnaba waliongea kwa uhodari zaidi, wakasema, “Ilikuwa ni lazima neno la Mungu liwafikieni nyinyi kwanza; lakini kwa kuwa mmelikataa na kujiona hamstahili uhai wa milele, basi, tunawaacheni na kuwaendea watu wa mataifa mengine.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

46 Ndipo Paulo na Barnaba wakawajibu kwa ujasiri, wakisema, “Ilitupasa kunena nanyi neno la Mungu kwanza. Lakini kwa kuwa mmelikataa, mkajihukumu wenyewe kuwa hamstahili uzima wa milele, sasa tunawageukia watu wa Mataifa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

46 Ndipo Paulo na Barnaba wakawajibu kwa ujasiri, wakisema, “Ilitupasa kunena nanyi neno la Mwenyezi Mungu kwanza. Lakini kwa kuwa mmelikataa, mkajihukumu wenyewe kuwa hamstahili uzima wa milele, sasa tunawageukia watu wa Mataifa.

Tazama sura Nakili




Matendo 13:46
37 Marejeleo ya Msalaba  

afadhali shikeni njia kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli.


Wakamwambia, Atawaangamiza wabaya wale; nae atawapangisha mizabibu wakulima wengine, watakaomlipa matunda kwa wakati wake.


Kwa sababu hii nawaambieni, ya kwamba ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu, na watapewa taifa lingine wenye kuzaa matunda yake.


Na hawo watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele: bali wenye haki katika uzima wa milele.


na mataifa yote wakhubiriwe kwa jina lake toba na ondoleo la dhambi, kuanzia Yerusalemi.


Alikuja kwake, nao walio wake hawakumpokea.


Ninyi mnaabudu msichokijua; sisi tunaabudu tukijuacho: kwa kuwa wokofu watoka kwa Wayahudi.


Lakini wao wakatoka Perga, wakapita kati ya inchi, wakafika Antiokia mji wa Pisidia, wakaingia katika sunagogi siku ya sabato, wakaketi.


Ndugu zangu, wana wa ukoo wa Ibrahimu, nao miongoni mwenu mnaomcha Mungu, kwenu ninyi neno la wokofu huu limepelekwa.


Na walipokuwa katika Salamini wakalikhubiri neno la Bwana katika masunagogi ya Wayahudi, nao walikuwa nae Yohana kuwakhudumia.


Lakini wengine walikaidi, wakakataa kuamini, wakiitukana ile Njia mbele ya mkutano; bassi, akaondoka akawaacha, akawatenga wanafunzi nao, akahujiana na watu killa siku katika darasa ya mtu mmoja, jina lake Tyranno.


Nae akaniambia, Enenda zako; kwa kuwa mimi nitakutuma mbali kwa watu wa mataifa.


hali kwanza niliwakhubiri wale wa Dameski na Yerusalemi, na katika inchi yote ya Yahudi, na watu wa mataifa, watubu wakamwelekee Mungu, wakiyatenda matendo yanayopatana na kutubu kwao.


Bassi ijulikane kwenu ya kwamba wokofu huu wa Mungu umepelekwa kwa mataifa, nao watasikia.


Mungu, akiisha kumfufua mtumishi wake Yesu, alimtuma kwenu ninyi kwanza, illi kuwabarikini kwa kumwepusha killa mmoja wenu na maovu wake.


Bassi walipoona ujasiri wa Petro na Yohana, na kujua ya kuwa ni watu wasio elimu, wasio maarifa, wakastaajabu, wakawatambua ya kwamba walikuwa pamoja na Yesu.


Enyi wenye shingo gumu, msiotahiriwa mioyo wala masikio, siku zote mnampinga Roho Mtakatifu; kama baba zenu walivyofanya na ninyi vivyo hivyo.


Marra akamkhubiri Yesu katika masunagogi, kwamba yeye ni Mwana wa Mungu.


kwa maana siionci haya Injili; kwa sababu ni uweza wa Mungu uuletao wokofu, kwa killa aaminiye, kwa Myahudi kwanza, hatta kwa Myunani pia.


bali utukufu na heshima na amani kwa killa mtu atendae mema, Myahudi kwanza na Myunani pia;


Na walio wengi wa ndugu walio katika Bwana, wakipata kuthubutika kwa ajili ya kufungwa kwangu, wamezidi sana kuthubutu kulinena neno la Bwana pasipo khofu.


walizima nguvu za moto, waliokoka na ukali wa upanga. Walitiwa nguvu baada va kuwa dhaifu, walikuwa hodari katika vita, walikimbiza majeshi ya wageni.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo