Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 13:45 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

45 Bali Wayahudi, walipowaona makutano, wakajaa wivu, wakayabisha maneno yaliyonenwa na Paolo, wakibisha na kutukana.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

45 Lakini Wayahudi walipoliona hilo kundi la watu walijaa wivu, wakapinga alichokuwa anasema Paulo na kumtukana.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

45 Lakini Wayahudi walipoliona hilo kundi la watu walijaa wivu, wakapinga alichokuwa anasema Paulo na kumtukana.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

45 Lakini Wayahudi walipoliona hilo kundi la watu walijaa wivu, wakapinga alichokuwa anasema Paulo na kumtukana.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

45 Lakini Wayahudi walipoona umati ule mkubwa wa watu, walijawa na wivu, wakayakanusha maneno Paulo aliyokuwa akisema.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

45 Lakini Wayahudi walipoona ule umati mkubwa wa watu walijawa na wivu, wakayakanusha maneno Paulo aliyokuwa akisema.

Tazama sura Nakili




Matendo 13:45
27 Marejeleo ya Msalaba  

Ole wenu waandisbi na Mafarisayo, wanafiki! kwa kuwa mnakula nyumba za wajane, na kwa unafiki mnasali sala ndefu; kwa hiyo mtapokea hukumu iliyo kubwa mno.


Kwa maana alijua ya kuwa wamemtoa kwa husuda.


Lakini Wayahudi wakawafitinisha wanawake watawa na watu wenye cheo na wakuu wa mji, wakawataharakisha watu wawaudhi Paolo na Barnaba; wakawatoa katika mipaka yao.


Wayahudi wakalika toka Antiokia na Ikonio, wakawashawishi makutano hatta wakampiga mawe Paolo wakamhurura nje ya mji, wakidhani ya kuwa amekwisha kufa.


Walakini Wayahudi wasioamini wakawataharakisha watu wa mataifa na kuwatia nia mbaya juu ya ndugu.


Lakini jamii ya watu wa mjini wakagawanyikana: bawa walikuwa upande wa Wayahudi, na hawa upande wa Mitume.


Hatta palipotokea shambulio la watu wa mataifa na Wayahudi pamoja na wakubwa wao juu yao, kuwatenda jeuri na kuwapiga mawe,


Na Wayahudi wasioamini wakaona wivu, wakajitwalia watu kadha wa kadha katika watu ovyo wasio na sifa njema wakakutanisha mkutano, wakafanya ghasia mjini, wakawaendea watu wa nyumba ya Yason wakataka kuwapeleka mbele ya watu wa mji;


Walipopingamana nae na kutukana, akakungʼuta mavazi yake, akawaambia, Damu yenu na iwe juu ya vichwa vyenu: mimi ni safi: langu sasa nitakwenda kwa watu wa mataifa.


Lakini wengine walikaidi, wakakataa kuamini, wakiitukana ile Njia mbele ya mkutano; bassi, akaondoka akawaacha, akawatenga wanafunzi nao, akahujiana na watu killa siku katika darasa ya mtu mmoja, jina lake Tyranno.


Akaondoka kuhani mkuu na wote waliokuwa pamoja nae (hao ndio walio wa madhehehu ya Masadukayo) wamejaa wivu,


wakijawa na udhalimu wa killa namna ya zina, na novu na tamaa na ubaya; wamejawa na husuda, na uuaji, na fitina, na khadaa;


Maana, ikiwa kwenu kuna husuda na fitina na faraka, je! si watu wa tabia za mwilini ninyi; tena mnaenenda kwa jinsi ya kibinadamu.


kwa kusafiri marra nyingi; khatari za mito; khatari za wanyangʼanyi; khatari kwa jamaa; khatari kwa mataifa; khatari za mijini; khatari za jangwani; khatari za baharini; khatari kwa ndugu za uwongo;


husuda, ulevi, ulafi, na yanayofanana na haya; juu ya haya nawaambieni mapema, kama nilivyokwisha kuwaambieni, watu watendao mambo ya jinsi hii hawatanrithi ufalme wa Mungu.


wakituzuia tusiseme na mataifa wapate kuokolewa; illi watimize dhambi zao siku zote; lakini hasira imewafikia hatta mwisho.


tena adha zangu na mateso yaliyonipata katika Antiokia, katika Ikonio, na katika Lustra; killa namna ya adha niliyoistahimili: nae Bwana akaniokoa katika yote.


Au mwadhani ya kwamba maandiko yasema burre? Roho ikaayo ndani yetu hutamani kiasi cha kuona wivu?


mambo ambayo wao huona kuwa ni ajabu ya ninyi kutokwenda mbio pamoja nao hatta ufisadi usio kiasi, wakiwatukaneni;


Lakini watu hawa huyatukana mambo wasiyoyajua, na mambo wayatambuayo kwa asili wajiharibu kwayo kama nyama wasio na akili.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo