Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 13:39 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

39 na kwa huyu killa amwaminiye huhesabiwa kuwa hana khatiya katika mambo yale asiyoweza kuhesabiwa kuwa hana khatiya kwa torati ya Musa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

39 na ya kwamba kila mmoja anayemwamini Yesu anasamehewa dhambi zote, jambo ambalo halingewezekana kwa njia ya sheria.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

39 na ya kwamba kila mmoja anayemwamini Yesu anasamehewa dhambi zote, jambo ambalo halingewezekana kwa njia ya sheria.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

39 na ya kwamba kila mmoja anayemwamini Yesu anasamehewa dhambi zote, jambo ambalo halingewezekana kwa njia ya sheria.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

39 Kupitia yeye, kila mtu amwaminiye anahesabiwa haki kwa kila kitu ambacho asingeweza kuhesabiwa haki kwa Torati ya Musa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

39 Kwa kupitia yeye, kila mtu amwaminiye anahesabiwa haki kwa kila kitu ambacho asingeweza kuhesabiwa haki kwa Torati ya Musa.

Tazama sura Nakili




Matendo 13:39
40 Marejeleo ya Msalaba  

Mwana sharia mmoja akasimama akimjaribu, akasema, Mwalimu, nifanyeni niurithi uzima wa milele?


Akamwambia, Umejibu vema; fanya hivi, ndipo utaishi.


Nawaambia ninyi, huyu alishuka nyumbani kwake amepata kibali kuliko yule: kwa maana killa ajikwezae atadhilika; nae ajidhiliye atakwezwa.


Kwa kuwa torati ilitolewa kwa mkono wa Musa, neema na kweli zilikuwa kwa mkono wa Yesu Kristo.


Amin, amin, nawaambieni, Alisikiae neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka ana uzima wa milele, wala hafiki hukumuni, bali amepita toka mauti hatta uzima.


Huyu manabii wote humshuhudia, ya kwamba kwa jina lake killa amwaminiye atapewa ondoleo la dhambi.


kwa maana kwa moyo watu huamini hatta kupata haki, na kwa kinywa hukiri hatta kupata wokofu.


Kwa maana Kristo ni mwisho wa sharia, illi killa aaminiye apate haki.


Twajua ya kuwa mambo yote yasemwayo na torati huyanena kwa hao walio chini ya torati, illi killa kinywa kifumbwe, ulimwengu wote ukapasiwe na hukumu ya Mungu:


kwa maana hapana mwenye mwili atakaehesabiwa kuwa na haki mbele za Mungu, kwa matendo ya sheria: kwa maanii kujua dhambi kabisa huja kwa njia ya sharia.


Kwa sababu sharia ndiyo ifanyayo hasira; maana pasipo sharia, hapana kosa.


bali na kwa ajili yetu sisi tutakaohesabiwa vivyo hivyo, sisi tunaomwamini yeye aliyemfufua Yesu katika wafu, Bwana wetu,


BASSI tukiisha kuhesabiwa wema utokao katika imani, tuwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo;


Sharia iliingia illi anguko lile liwe kubwa sana; na dhambi ilipozidi, neema ilikuwa nyingi zaidi;


Bassi zaidi sana tukiisha kupewa haki katika damu yake tutaokolewa na ghadhabu kwa yeye.


SASA, bassi, hapana hukumu juu yao walio katika Kristo Yesu, wasioenenda kwa kufuata mambo ya mwili bali mambo ya roho.


Maana yale yasiyowezekana kwa sharia, kwa kuwa dhaifu kwa sababu ya mwili, Mungu, kwa kumtuma Mwana wake mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa ajili ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili:


bali Israeli wakiifuata sharia ya haki hawakuifikilia ile sharia.


Na baadhi yenu mlikuwa watu wa namna hizi; lakini mlioshwa, lakini mlitakaswa, lakini mlihesabiwa kuwa na haki katika jina la Bwana Yesu na katika Roho ya Mungu wetu.


tukijua ya kuwa mwana Adamu hafanyiziwi wema kwa matendo ya sharia, hali kwa imani ya Yesu Kristo, sisi tulimwamini Yesu Kristo illi tufauyiziwe wema kwa imani ya Kristo, wala si kwa matendo ya sharia; maana kwa matendo ya sharia hapana mwenye mwili atakaefanyiziwa wema.


Maana mimi kwa sharia naliifia sharia illi nimwishie Mungu.


Na andiko, likiona tangu zamani kwamba Mungu atawafanyizia mataifa wema kwa imani, lilimkhubiri Ibrahimu Injili zamani, ya kama, Kwa wewe mataifa yote yatabarikiwa.


Tena namshuhudia killa mtu atahiriwae, kwamba ni wajibu wake kuitimiza sharia yote.


Na killa kuhani husimama killa siku akifanya ibada, akitoa dhabihu zilezile marra nyingi; nazo haziwezi kabisa kuondoa dhambi.


Maana haiyumkini damu ya mafahali na mbuzi iondoe dhambi.


(kwa maana sharia ile haikukamilisha neno); na pamoja na haya kuliingizwa matumaini yaliyo mazuri zaidi, ambayo kwayo twamkaribia Mungu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo