Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 13:27 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

27 Kwa maana wakaao Yerusalemi, na wakuu wao, kwa kuwa hawakumjua huyu, wala sauti za manabii wanaosomwa killa sabato, wamezitimiza kwa kumhukumu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

27 Kwa maana wenyeji wa Yerusalemu na wakuu wao hawakumtambua yeye kuwa Mwokozi, wala hawakuelewa maneno ya manabii yanayosomwa kila Sabato. Hata hivyo, waliyafanya maneno ya manabii yatimie kwa kumhukumu Yesu adhabu ya kifo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

27 Kwa maana wenyeji wa Yerusalemu na wakuu wao hawakumtambua yeye kuwa Mwokozi, wala hawakuelewa maneno ya manabii yanayosomwa kila Sabato. Hata hivyo, waliyafanya maneno ya manabii yatimie kwa kumhukumu Yesu adhabu ya kifo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

27 Kwa maana wenyeji wa Yerusalemu na wakuu wao hawakumtambua yeye kuwa Mwokozi, wala hawakuelewa maneno ya manabii yanayosomwa kila Sabato. Hata hivyo, waliyafanya maneno ya manabii yatimie kwa kumhukumu Yesu adhabu ya kifo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

27 Kwa sababu watu wa Yerusalemu na viongozi wao hawakumtambua, wala kuelewa maneno ya manabii yanayosomwa kila Sabato, bali waliyatimiza maneno hayo kwa kumhukumu yeye.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

27 Kwa sababu wakaao Yerusalemu na viongozi wao hawakumtambua wala kuelewa maneno ya manabii yasomwayo kila Sabato, bali waliyatimiza maneno hayo kwa kumhukumu yeye.

Tazama sura Nakili




Matendo 13:27
25 Marejeleo ya Msalaba  

Yesu akajihu, akawaamhia, Mwajidanganya, kwa kuwa hamyajui maandiko wala uweza wa Mungu.


Akasema, Nakuambia, Petro, jogoo hatawika leo, kabla hujanikana marra tatu kwamba hunijui.


Pilato akawaita pamoja makuhani wakuu, na wakubwa, na watu, akawaambia,


na jinsi makuhani wakuu na wakubwa wetu walivyomtoa kwa hukumu ya kufa, wakamsulibisha;


Lakini haya yote watawatenda kwa sababu ya jina langu, kwa kuwa hawamjui aliyenipeleka.


Na hayo watawatendeni kwa sababu hawakumjua Baba wala mimi.


Mwayachunguza maandiko, kwa sababu mnadhani kwamba ninyi mna uzima wa milele ndani yake: na hayo ndiyo yanayonishuhudia:


Bassi Yesu akawaambia, Mtakapokuwa mmekwisha kumwinua Mwana wa Adamu, ndipo mtakapofahamu ya kuwa mimi ndiye, na ya kuwa sifanyi neno kwa nafsi yangu tu, illa kama Baba yangu alivyonifundisha, ndivyo nisemavyo.


Kwa maana tangu zamani za kale Musa anao watu wakhubirio mambo yake; katika killa mji husomwa killa siku katika masunagogi.


Wakiislia kuwekana kwa siku, wakaja kwake nyumbani kwake, watu wengi sana, akawaeleza kwa taratibu na kuushuhudia ufalme wa Mungu, akiwaonya mambo yake Yesu, kwa maneno ya sharia ya Musa na ya manabii, tangu assubuhi hatta jioni.


Bassi sasa ndugu, najua ya kuwa mliyatenda haya kwa kutokujua kwenu, kama na wakuu wenu walivyotenda.


Kwa maana sitaki ndugu msiijue siri hii, ms jione kuwa wenye akili, ya kwamba kwa sehemu ugumu umewapata Israeli, mpaka ntimilifu wa mataifa uwasili;


ambayo wenye kutawala dunia hii hawakuijua hatta mmoja; maana kama wangaliijua, wasingalimsulibisha Bwana wa utukufu;


pamoja na hayo fikara zao zilitiwa ugumu; kwa maana hatta leo utaji huo huo, wakati lisomwapo Agano la Kale, wakaa, haukuondolewa; ambao buoudolewa katika Kristo;


ambao mungu wa dunia hii amepofusha akili za wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu.


mimi niliyekuwa kwanza mtukanaji, mwenye kuudhi watu, mwenye jeuri: lakini nalirehemiwa kwa kuwa nalitenda hivyo kwa njinga, na kwa kutokuwa na imani;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo