Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 13:25 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

25 Nae Yohana alipokuwa akimaliza mwendo wake alinena, Mwanidhani mimi kuwa nani? Mimi siye. Lakini, angalieni, anakuja mmoja nyuma yangu ambae mimi sistahili kumlegezea viatu vya miguu yake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

25 Yohane alipokuwa anamaliza ujumbe wake aliwaambia watu: ‘Mnadhani mimi ni nani? Mimi si yule mnayemtazamia. Huyo anakuja baada yangu na mimi sistahili hata kuzifungua kamba za viatu vyake.’

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

25 Yohane alipokuwa anamaliza ujumbe wake aliwaambia watu: ‘Mnadhani mimi ni nani? Mimi si yule mnayemtazamia. Huyo anakuja baada yangu na mimi sistahili hata kuzifungua kamba za viatu vyake.’

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

25 Yohane alipokuwa anamaliza ujumbe wake aliwaambia watu: ‘Mnadhani mimi ni nani? Mimi si yule mnayemtazamia. Huyo anakuja baada yangu na mimi sistahili hata kuzifungua kamba za viatu vyake.’

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

25 Yahya alipokuwa anakamilisha kazi yake, alisema: ‘Ninyi mnadhani mimi ni nani? Mimi si yeye. La, lakini yeye yuaja baada yangu, ambaye mimi sistahili kufungua kamba za viatu vya miguu yake.’

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

25 Yahya alipokuwa anakamilisha kazi yake, alisema: ‘Ninyi mnadhani mimi ni nani? Mimi si yeye. La hasha, lakini yeye yuaja baada yangu, ambaye mimi sistahili kufungua kamba za viatu vya miguu yake.’

Tazama sura Nakili




Matendo 13:25
19 Marejeleo ya Msalaba  

Mimi nawabatizeni katika maji mpate kutubu: bali yeye ajae nyuma yangu ni hodari kuliko mimi, wala sistahili hatta kuchukua viatu vyake; yeye atawabatizeni kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.


Akakhubiri akinena, Yuaja nyuma yangu aliye hodari kuliko mimi, ambae kwamba sistabili kuinama na kuzifungua kanda za viatu vyake.


Siku ya pili yake Yohana amwona Yesu anakuja kwake, akanena, Tazama, Mwana Kondoo wa Mungu, aichukuae dhambi ya ulimwengu!


Nami nimeona, tena nimeshuhudia ya kuwa huyu ni Mwana wa Mungu.


Akamtazama Yesu, akitembea, akasema, Tazama, Mwana Kondoo wa Mungu!


Yesu akawaambia, Chakula changu ndicho hiki, niyatende mapenzi yake aliyenipeleka nikaimalize kazi yake.


Yeye anenae kwa nafsi yake tu, hutafuta utukufu wake mwenyewe; bali yeye anaetafuta utukufu wake aliyempeleka, huyu ni wa kweli wala ndani yake hamna udhalimu.


Kwa maana Daud, akiisha kulitumikia shauri la Mungu katika kizazi chake, alilala, akawekwa pamoja na baba zake, akaona uharibifu.


Paolo akasema, Yohana alibatiza kwa ubatizo wa toba, akiwaambia watu wamwamini yeye atakaekuja nyuma yake, yaani Kristo Yesu.


Lakini siyahesabu maisha yaugu kuwa kitu cha thamani kwangu kama kuumaliza mwendo wangu na khuduma ile niliyopokea kwa Bwana Yesu, kuishuhudia Injili ya neema ya Mungu.


Kwa maana hatujikhubiri nafsi zetu, hali Kristo Yesu Bwana; na sisi wenyewe kuwa watumishi wenu kwa ajili ya Kristo.


Nimevifanya vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda;


Hatta watakapoumaliza ushuhuda wao yule nyama atokae katika abuso atafanya vifa nao, nae atawashinda na kuwaua.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo