Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 13:2 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

2 Bassi hawa walipokuwa wakimkhudumia Bwana na kufunga, Roho Mtakatifu akasema, Niwekeeni Barnaba na Saul kwa kazi ile niliyowaitia.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 Walipokuwa wanafanya ibada yao kwa Bwana na kufunga, Roho Mtakatifu akasema: “Niteulieni Barnaba na Saulo kwa ajili ya kazi niliyowaitia.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

2 Walipokuwa wanafanya ibada yao kwa Bwana na kufunga, Roho Mtakatifu akasema: “Niteulieni Barnaba na Saulo kwa ajili ya kazi niliyowaitia.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 Walipokuwa wanafanya ibada yao kwa Bwana na kufunga, Roho Mtakatifu akasema: “Niteulieni Barnaba na Saulo kwa ajili ya kazi niliyowaitia.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 Walipokuwa wakimwabudu Mwenyezi Mungu na kufunga, Roho Mtakatifu wa Mungu akasema, “Nitengeeni Sauli na Barnaba kwa kazi niliyowaitia.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 Walipokuwa wakimwabudu Mwenyezi Mungu na kufunga, Roho wa Mwenyezi Mungu akasema, “Nitengeeni Sauli na Barnaba kwa kazi ile maalum niliyowaitia.”

Tazama sura Nakili




Matendo 13:2
41 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini namna hii haitoki illa kwa kusali na kufunga.


Tena mfungapo, msiwe kama wanafiki wenye uso wa kukunjamana: maana hujiumbua nyuso zao, illi waonekane na watu kuwa wanafunga. Amin, nawaambieni, wamekwisha kupata thawabu yao.


Bassi mwombeni Bwana wa mavuno, apeleke watenda kazi katika mavuno yake.


BASSI baada ya mambo haya Bwana akachagua wengine sabaini, akawatuma wawili wawili wamtangulie kwenda killa mji na pahali atakakokwenda mwenyewe.


nae mjane wa miaka themanini na mine; asiyeondoka hekaluni, kwa kufunga na kusali akiabudu usiku na mchana.


Na Petro alikuwa akiyafikiri yale maono. Roho akamwambia, Wako watu watatu wanakutaka.


Kornelio akanena, Leo ni siku ya nne tangu nilijiokuwa nikifunga hatta saa hii: na saa tissa nalikuwa nikisali nyumbani mwangu: kumbe! mtu amesimama mbele yangu, mwenye nguo zingʼaazo, akasema,


Ndipo, wakiisha kuomba na kufunga, wakaweka mikono yao juu yao, wakawaacha waende zao.


Bassi watu hao, wakiisha kupelekwa na Roho Mtakatifu wakatelemkia Selukia, na kutoka huko wakasafiri baharini hatta Kupro.


Na kutoka huko wakasafiri baharini kwenda Antiokia. Huko ndiko walikoombewa neema ya Mungu kwa ile kazi waliyokwisha kuitimiza.


Jiangalieni nafsi zenu, na kundi lote, ambalo Roho Mtakatifu aliwakabidhi mlisimamie, kanisa lake Mungu, alilojipatia kwa damu yake mwenyewe.


Nae akaniambia, Enenda zako; kwa kuwa mimi nitakutuma mbali kwa watu wa mataifa.


Na Yusuf, aliyeitwa na mitume Barnaba (tafsiri yake, Mwana wa faraja), Mlawi, asili yake ni mtu wa Kupro,


na sisi tutadumu katika kumwomba Mungu na kulikhudumia Neno lake.


Roho akamwambia Filipo, Sogea karibu na gari bili, ukashikamane nalo.


Lakini Bwana akamwambia, Shika njia; kwa maana huyu ni chombo kiteule kwangu, alichukue Jina langu mbele ya mataifa, na wafalme, na wana wa Israeli.


PAOLO, mtumwa wa Yesu Kristo, aliyeitwa kuwa mtume, na kuwekwa aikhubiri Injili ya Mungu,


Tena wakhubirije, wasipopelekwa? Kama ilivyoandikwa, Ni mizuri namna gani miguu yao wakhubirio khabari ya mema.


illi niwe kuhani wa Yesu Kristo katika watu wa mataifa, niifanyie Injili ya Mungu kazi ya ukuhani, kusudi mataifa wawe sadaka yenye kibali, ikiisha kutakaswa na Roho Mtakatifu.


lakini kazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja, yule yule, akimgawia killa mmoja peke yake kama apendavyo yeye.


Msinyimane isipokuwa mmepatana kwa muda, illi mpate faragha kwa kufunga na kuomba, mkajiane tena, Shetani asije akawajarihu kwa kutokuwa na kiasi kwenu.


kwa kazi na kusumbuka; kwa kukesha marra nyingi; kwa njaa na kiu; kwa kufunga marra nyingi; kwa baridi na kuwa uchi.


kafika mapigo, katika vifungo, katika fitina, katika kazi, katika kukesha, katika kufunga;


Lakini Mungu aliyenitenga tangu tumboni mwa mama yangu, akaniita kwa neema yake,


ambayo nilifanywa mkhudumu wake, kwa kadiri ya kipawa cha neema yake Mungu niliyopewa kwa kadiri ya kutenda kazi kwa uweza wake.


Mwambieni Arkippo, Iangalie sana khuduma ile uliyopewa katika Bwana, illi uitimize.


kwa ajili ya huo naliwekwa niwe mkhubiri na mtume (nasema kweli katika Kristo, sisemi uwongo), mwalimu wa mataifa katika imani na kweli.


aliyonifauya mkhubiri na mtume na mwalimu wa mataifa.


Na yale uliyoyasikia kwangu kwa mashahidi wengi, uwakabidbi hayo watu waaminifu watakaofaa kuwafundisha na wengine.


Luka peke yake yupo hapa pamoja nami. Umtwae Marko, umlete pamoja nawe; maana anifaa kwa kazi ya khuduma.


Bali wewe erevuka katika yote, vumilia mabaya, fanya kazi ya mwinjilisti, timiliza khuduma yako.


Na hapana mtu ajitwaliae heshima hii, illa yeye aitwae na Mungu kama vile Harimi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo