Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 13:15 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

15 Kiisha baada ya kusomwa torati na chuo cha manabii, wakuu wa sunagogi wakatuma mtu kwao, na kuwaambia, Ndugu, kama mkiwa na neno la kuwafaa watu hawa, lisemeni.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

15 Baada ya masomo katika kitabu cha sheria ya Mose na katika maandiko ya manabii, wakuu wa lile sunagogi waliwapelekea ujumbe huu: “Ndugu, kama mnalo jambo la kuwaambia watu ili kuwapa moyo, semeni.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

15 Baada ya masomo katika kitabu cha sheria ya Mose na katika maandiko ya manabii, wakuu wa lile sunagogi waliwapelekea ujumbe huu: “Ndugu, kama mnalo jambo la kuwaambia watu ili kuwapa moyo, semeni.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

15 Baada ya masomo katika kitabu cha sheria ya Mose na katika maandiko ya manabii, wakuu wa lile sunagogi waliwapelekea ujumbe huu: “Ndugu, kama mnalo jambo la kuwaambia watu ili kuwapa moyo, semeni.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

15 Baada ya Torati ya Musa na Kitabu cha Manabii kusomwa, viongozi wa sinagogi wakawatumia ujumbe wakisema, “Ndugu, kama mna neno la kuwafariji watu hawa, tafadhali lisemeni.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

15 Baada ya Torati ya Musa na Kitabu cha Manabii kusomwa, viongozi wa sinagogi wakawatumia ujumbe wakisema, “Ndugu, kama mna neno la kuwafariji watu hawa, tafadhali lisemeni.”

Tazama sura Nakili




Matendo 13:15
21 Marejeleo ya Msalaba  

Kumbe! akaja mtu mmoja katika wakuu wa sunagogi, jina lake Yairo: hatta alipomwona, akaanguka miguuni pake,


Torati na manabii zilikuwako mpaka Yohana. Tangu wakati ule, khabari njema ya ufalme wa Mungu inakhubiriwa, na killa mtu anauingia kwa nguvu.


Ndugu imepasa andiko litimizwe, alilolinena Roho Mtakatifu zamani kwa kinywa cha Daud, katika khabari za Yuda, aliyekuwa kiongozi wao waliomkamata Yesu: kwa sababu alikuwa amehesabiwa pamoja na sisi,


Kwa maana wakaao Yerusalemi, na wakuu wao, kwa kuwa hawakumjua huyu, wala sauti za manabii wanaosomwa killa sabato, wamezitimiza kwa kumhukumu.


Kwa maana tangu zamani za kale Musa anao watu wakhubirio mambo yake; katika killa mji husomwa killa siku katika masunagogi.


Na baada ya hoja nyingi Petro akasimama, akawaambia, Ndugu zangu, ninyi mnajua ya kuwa siku za kwanza Mungu alichagua miongoni mwetu mataifa walisikie neno la Injili kwa kinywa changu, na kuliamini.


Na Wayunani wote wakamshika Sosthene, mkuu wa sunagogi, wakampiga mbele ya kiti cha hukumu. Na Gallio hakuyaona mambo hayo kuwa kitu.


Na Krispo, mkuu wa sunagogi, akamwamini Bwana pamoja na nyumba yake yote. Wakorintho wengi wakasikia, wakaamini, wakabatizwa.


Ndugu, mniwie radhi, niseme pasipo khofu mbele yenu khabari za baba yetu mkuu Daud, ya kuwa alifariki akazikwa, na kaburi lake liko kwetu hatta leo.


Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?


Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha mbalimbali, kama Roho alivyowajalia kutamka.


Na, akiisha kupita pande zile na kuwafariji kwa maneno mengi, akafika Uyunani.


ENYI wanaume, ndugu zangu ua baba zangu, nisikilizeni, nikijitetea nafsi yangu mbele yemi sasa.


Na Yusuf, aliyeitwa na mitume Barnaba (tafsiri yake, Mwana wa faraja), Mlawi, asili yake ni mtu wa Kupro,


Nae akasema, Ndugu zangu na baba zangu, sikilizeni: Mungu wa utukufu alimtokea baba yetu Ibrahimu, alipokuwa katika Mesopotamia, kabla hajakaa Kharran, akamwambia,


mwenye kuonya, katika kuonya kwake; mwenye kukarimu, kwa moyo mweupe; mwenye kusimamia, kwa bidii; mwenye kurehemu, kwa furaha.


Bali yeye akhutubuye, anena na watu maneno ya kuwajenga, na kuwafariji, na kuwatia moyo.


pamoja na hayo fikara zao zilitiwa ugumu; kwa maana hatta leo utaji huo huo, wakati lisomwapo Agano la Kale, wakaa, haukuondolewa; ambao buoudolewa katika Kristo;


Kwa maana maonyo yetu siyo ya ukosefu wala ya uchafu, wala ya hila,


Nawasihini, ndugu, livumilieni neno hili lenye maonyo; maana nimewaandikia kwa maneno machache.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo