Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 13:1 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 NA huko Antiokia katika kanisa lililokuwako palikuwa na manabii na waalimu, Barnaba na Sumeon aitwae Niger, na Lukio Mkurene, na Manaen aliyekuwa ndugu wa kunyonya wa Herode mfalme, na Saul.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Katika kanisa la Antiokia kulikuwa na watu wengine waliokuwa manabii na waalimu; miongoni mwao wakiwa Barnaba, Simoni aitwaye pia Mweusi, Lukio wa Kurene, Manaeni ambaye alikuwa amelelewa pamoja na mfalme Herode, na Saulo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Katika kanisa la Antiokia kulikuwa na watu wengine waliokuwa manabii na waalimu; miongoni mwao wakiwa Barnaba, Simoni aitwaye pia Mweusi, Lukio wa Kurene, Manaeni ambaye alikuwa amelelewa pamoja na mfalme Herode, na Saulo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Katika kanisa la Antiokia kulikuwa na watu wengine waliokuwa manabii na waalimu; miongoni mwao wakiwa Barnaba, Simoni aitwaye pia Mweusi, Lukio wa Kurene, Manaeni ambaye alikuwa amelelewa pamoja na mfalme Herode, na Saulo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Katika kundi la waumini wa Isa huko Antiokia kulikuwa na manabii na walimu: Barnaba, Simeoni aitwaye Nigeri, Lukio Mkirene, Manaeni aliyekuwa amelelewa pamoja na Mfalme Herode Agripa, na Sauli.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Katika kundi la waumini huko Antiokia ya Shamu walikuwako manabii na walimu: yaani Barnaba, Simeoni aitwaye Nigeri, Lukio Mkirene, Manaeni aliyekuwa amelelewa pamoja na Mfalme Herode Agripa, na Sauli.

Tazama sura Nakili




Matendo 13:1
34 Marejeleo ya Msalaba  

Hatta walipokuwa wakitoka humo, wakakutana na mtu Mkurene, jina lake Simon; huyu wakamtumikisha auchukue msalaba wake.


HATTA katika mwaka wa kumi na tano wa kutawala kwake Tiberio Kaisari, Pontio Pilato alipokuwa liwali wa Yahudi, na Herode tetrarka wa Galilaya, na Filipo ndugu yake tetrarka wa Iturea, na wa inchi ya Trakoniti, na Lusania tetrarka wa Abilene,


Wakafanya hivyo, wakawapelekea wazee kwa mikono ya Barnaha na Saul.


Na Barnaba na Saul, walipokwisha kuitimiza khuduma yao, wakarejea kutoka Yerusalemi wakamchukua pamoja nao Yohana aitwae Marko.


Lakini Saul ambae ndiye Paolo, akijaa Roho Mtakatifu, akamkazia macho, akanena,


Tena Yuda na Sila, kwa kuwa wao wenyewe ni manabii, wakawausia ndugu kwa maneno mengi, wakawathubutisha.


Na Paolo na Barnaba wakakaa huko Antiokia, wakifundisiia na kulikhubiri neno la Bwana, pamoja na watu wengine wengi.


Na Paolo, alipokwisba kuweka mikono yake juu yao, Roho Mtakatifu akaja juu yao wakaanza kunena kwa lugha, na kutabiri.


Mtu huyu alikuwa na binti wane, mabikira, waliotabiri.


Na Yusuf, aliyeitwa na mitume Barnaba (tafsiri yake, Mwana wa faraja), Mlawi, asili yake ni mtu wa Kupro,


LAKINI Saul, akizidi kutisha na kuwaza kuwaua wanafunzi wa Bwana, akamwendea kuhani mkuu,


Timotheo, mtenda kazi pamoja nami, awasalimu, na Lukio, na Yason, na Sosipatro, jamaa zangu.


Killa mwanamume, asalipo, au atoapo unabii, nae ana kitu kichwani, yuaibisha kichwa chake.


Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama simi upendo, si kitu mimi.


Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika.


Na manabii wanene wawili, au watatu, na wengine wapamhanue.


Na roho za manabii huwatii manabii.


Au je! ni mimi peke yangu na Barnaba tusio na uwezo kutokufanya kazi?


Na Wayahudi wakajigeuza pamoja nae, hatta Barnaba nae akachukuliwa na unafiki wao.


tena walipokwisha kuijua neema niliyopewa, Yakobo, na Kefa, na Yohana, wenye sifa kuwa ni nguzo, walinipa mimi na Barnaba mkono wa kuume wa shirika, illi sisi tuende kwa mataifa, na wao waende kwa watu wa tohara;


Na yeye aliwatoa wengine kuwa mitume; na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti, na wengine kuwa wachungaji, na waalimu,


Watakatifu wote wawasalimu, khassa wao walio wa nyumba ya Kaisari.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo