Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 11:28 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

28 Akasimama mmojawapo wao, jina lake Agabo, akaonyesha kwa nweza wa Roho Mtakatifu kwamba njaa kubwa itakuja karibu katika dunia nzima; nayo ikatukia katika siku za Klaudio Kaisari.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

28 Basi, mmoja wao aitwaye Agabo alisimama, na kwa uwezo wa Roho akabashiri kwamba kutakuwa na njaa kubwa katika nchi yote. (Njaa hiyo ilitokea wakati wa utawala wa Klaudio).

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

28 Basi, mmoja wao aitwaye Agabo alisimama, na kwa uwezo wa Roho akabashiri kwamba kutakuwa na njaa kubwa katika nchi yote. (Njaa hiyo ilitokea wakati wa utawala wa Klaudio).

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

28 Basi, mmoja wao aitwaye Agabo alisimama, na kwa uwezo wa Roho akabashiri kwamba kutakuwa na njaa kubwa katika nchi yote. (Njaa hiyo ilitokea wakati wa utawala wa Klaudio).

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

28 Mmoja wao aliyeitwa Agabo akasimama, akatabiri kwa uweza wa Roho Mtakatifu wa Mungu kwamba njaa kubwa ingeenea ulimwengu mzima. (Njaa hiyo ilitokea wakati wa utawala wa Klaudio.)

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

28 Mmoja wao, jina lake Agabo, akasimama akatabiri kwa uweza wa Roho wa Mwenyezi Mungu kwamba njaa kubwa itaenea ulimwengu mzima. Njaa hiyo ilitokea wakati wa utawala wa Klaudio.

Tazama sura Nakili




Matendo 11:28
10 Marejeleo ya Msalaba  

Na injili hii ya ufalme itakhubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; ndipo ule mwisho utakapokuja.


Maana taifa litaondoka kupigana na taifa, na ufalme kupigana na ufalme; kutakuwako na njaa, na maradhi, na matetemeko ya inchi pahali pahali.


HATTA siku zile kulitoka amri kwa Kaisari Augusto ya kama iandikwe orodha ya majina ya walimwengu wote:


HATTA katika mwaka wa kumi na tano wa kutawala kwake Tiberio Kaisari, Pontio Pilato alipokuwa liwali wa Yahudi, na Herode tetrarka wa Galilaya, na Filipo ndugu yake tetrarka wa Iturea, na wa inchi ya Trakoniti, na Lusania tetrarka wa Abilene,


Akamwona Myahudi mmoja, jina lake Akula, mzalia wa Ponto; nae amekuja kutoka inchi ya italia siku za karibu, pamoja na Priskilla mkewe, kwa sababu Klaudio amewaamuru Wayahudi wote watoke Rumi.


Bassi tulipokuwa tukikaa huko siku nyingi, nabii mmoja jina lake Agabo akashuka kutoka Yahudi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo