Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 11:23 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

23 Nae, alipokwisha kufika na kuiona neema ya Mungu akafurahi, akawasihi wote waambatane na Bwana kwa kusudi la moyo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

23 Alipofika huko na kuona jinsi Mungu alivyowaneemesha wale watu, alifurahi na kuwahimiza wote wadumu katika uaminifu wao kwa Bwana.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

23 Alipofika huko na kuona jinsi Mungu alivyowaneemesha wale watu, alifurahi na kuwahimiza wote wadumu katika uaminifu wao kwa Bwana.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

23 Alipofika huko na kuona jinsi Mungu alivyowaneemesha wale watu, alifurahi na kuwahimiza wote wadumu katika uaminifu wao kwa Bwana.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

23 Alipofika na kuona madhihirisho ya neema ya Mungu, akafurahi na kuwatia moyo waendelee kuwa waaminifu kwa Bwana Isa kwa mioyo yao yote.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

23 Alipofika na kuona madhihirisho ya neema ya Mwenyezi Mungu, akafurahi na kuwatia moyo waendelee kuwa waaminifu kwa Bwana Isa kwa mioyo yao yote.

Tazama sura Nakili




Matendo 11:23
37 Marejeleo ya Msalaba  

Wakati huo Yesu aliwaambia wanafunzi wake, Mtu atakae kuandama nyuma yangu, ajikane nafsi yake, ajitwike msalaba wake, anifuate.


Yesu, alipoiona imani yao, akamwambia yule mwenye kupooza, Mwanangu, dhambi zako zimeondolewa.


Kaeni ndani yangu, na mimi ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu, kadhalika na ninyi, msipokaa ndani yangu.


Sunagogi lilipofumukana, Wayahudi wengi na waongofu watawa wakashikamana na Paolo na Barnaba; nao, wakisema nao, wakawatia moyo kudumu katika neema ya Mungu.


wakifanya imara roho za wanafunzi na kuwaonya wakae katika imani, na ya kwamba imetupasa kuingia katika ufalme wa Mungu kwa njia ya shidda nyingi.


Na kutoka huko wakasafiri baharini kwenda Antiokia. Huko ndiko walikoombewa neema ya Mungu kwa ile kazi waliyokwisha kuitimiza.


Paolo akamchagua Sila akaondoka, akiombewa na wale ndugu, apewe neema ya Mungu.


Lakini siyahesabu maisha yaugu kuwa kitu cha thamani kwangu kama kuumaliza mwendo wangu na khuduma ile niliyopokea kwa Bwana Yesu, kuishuhudia Injili ya neema ya Mungu.


Bassi, sasa ndugu, nawawekeni katika mikono ya Mungu, na kwa neno la neema yake, kwake yeye awezae kuwajengeni na kuwapeni urithi pamoja nao wote waliotakasika.


Na Yusuf, aliyeitwa na mitume Barnaba (tafsiri yake, Mwana wa faraja), Mlawi, asili yake ni mtu wa Kupro,


mwenye kuonya, katika kuonya kwake; mwenye kukarimu, kwa moyo mweupe; mwenye kusimamia, kwa bidii; mwenye kurehemu, kwa furaha.


Bassi, ndugu wapendwa, mwe imara, msiotikisika, mkizidi sana kutenda kazi ya Bwana siku zote, kwa kuwa taabu yenu siyo burre katika Bwana.


Bassi, nilipokusudia haya nalitumia kigeugeu; au niyakusudiayo, nayakusudia kwa jinsi ya mwili illi iwe hivi kwangu, kusema ndiyo, ndiyo, na siyo, siyo?


NASI tukitenda kazi pamoja nae tunakusihini msiipokee neema ya Mungu burre,


iliyofika kwenu, kama ilivyo katika ulimwengu wote, ikizaa matunda na kukua, kama na inavyokua kwenu, tangu siku mliposikia nikaifahamu sana neema ya Mungu katika kweli;


Bali wewe umeyafuata mafundisho yangu, na mwenendo wangu, na makusudi yangu, na imani, na upole, na upendo, na uvumilivu,


Kwa mkono wa Silwano, ndugu mwaminifu kama nionavyo, nimewaandikieni kwa maneno machache, nikionya na kushuhudia ya kuwa hii ndiyo neema ya kweli va Mungu. Simameni imara katika hiyo.


Na sasa, watoto wadogo, kaeni ndani yake, illi, atakapofunuliwa, tuwe na ujasiri, wala tusiaibishwe mbele zake katika kuja kwake.


Sina furaha iliyo kuu kuliko hii, kusikia ya kwamba watoto wangu wanakwenda katika kweli.


Kwa maana kuna watu wamejiingiza kwa siri, watu walioandikiwa zamani hukumu hii, makafiri, wabadilio neema ya Mungu wetu kuwa ufasiki, nao humkana yeye aliye peke yake Mola, na Bwana wetu Yesu Kristo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo