Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 11:16 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

16 Nikalikumbuka neno lile la Bwana, jinsi alivyosema, Yohana alibatiza kwa maji, bali ninyi mtabatizwa kwa Roho Mtakatifu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 Hapo nilikumbuka yale maneno Bwana aliyosema: ‘Yohane alibatiza kwa maji, lakini nyinyi mtabatizwa kwa Roho Mtakatifu.’

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 Hapo nilikumbuka yale maneno Bwana aliyosema: ‘Yohane alibatiza kwa maji, lakini nyinyi mtabatizwa kwa Roho Mtakatifu.’

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 Hapo nilikumbuka yale maneno Bwana aliyosema: ‘Yohane alibatiza kwa maji, lakini nyinyi mtabatizwa kwa Roho Mtakatifu.’

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 Nami nikakumbuka yale Bwana Isa aliyosema, ‘Yahya alibatiza kwa maji, lakini ninyi mtabatizwa katika Roho wa Mungu.’

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 Nami nikakumbuka neno la Bwana Isa alivyosema, ‘Yahya alibatiza kwa maji, lakini ninyi mtabatizwa katika Roho wa Mwenyezi Mungu.’

Tazama sura Nakili




Matendo 11:16
20 Marejeleo ya Msalaba  

Mimi nawabatizeni katika maji mpate kutubu: bali yeye ajae nyuma yangu ni hodari kuliko mimi, wala sistahili hatta kuchukua viatu vyake; yeye atawabatizeni kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.


wakabatizwa nae mtoni Yordani, wakiziungama dhambi zao.


Mimi naliwabatizeni kwa maji; bali yeye atawabalizeni kwa Roho Mtakatifu.


Wakakumbuka maneno yake,


Yohana akajibu, akawaambia wote, Mimi nawabatiza kwa maji, lakini yuaja aliye hodari kuliko mimi, ambae kwamba mimi sistahili kumfungulia ukanda wa viatu vyake; yeye atawabatizeni kwa Roho Mtakatifu na kwa moto:


Yohana akawajibu akanena, Mimi nabatiza kwa maji: kati mwenu amesimama msiyemjua ninyi.


Nami sikumjua, lakini yeye aliyenipeleka kubatiza kwa maji, huyu aliniambia, Yeye ambae utakaemwona Roho akishuka na kukaa juu yake, huyu ndiye abatizae kwa Roho Mtakatifu.


Lakini Mfariji, Roho Mtakatifu, ambae Baba atampeleka kwa jina langu, yeye atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.


Lakini nimewaambieni haya, illi kusudi saa ile itakapokuja myakumbuke ya kuwa mimi naliwaambieni. Haya sikuwaambieni tangu mwanzo, kwa sababu nalikuwa pamoja nanyi.


ya kwamba Yohana alibatiza kwa maji, bali ninyi mtabatizwa katika Roho Mtakatifu baada ya siku hizi si nyingi.


Nimewapeni mfano katika mambo yote ya kuwa kwa kushika kazi hivi imewapaseni kuwasaidia wasio na nguvu, na kuyakumbuka maneno ya Bwana Yesu, jinsi alivyosema mwenyewe, Ni kheri kutoa kuliko kupokea.


Kwa maana katika Roho mmoja sisi sote tulibatizwa tukaingia katika mwili mmoja, ikiwa tu Wayahudi, au ikiwa tu Wayunani; ikiwa tu watumwa au ikiwa tu huru; nasi sote tulinyweshwa Roho mmoja.


WAPENZI, waraka huu ndio wa pili niwaandikiao ninyi; katika hizo naziamsha nia zenu sali kwa kuwakumbusheni,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo