Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 10:45 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

45 Na wale waliotahiriwa walioamini, wakashangaa, watu wote waliokuja pamoja na Petro, kwa sababu mataifa nao wameshukiwa kipaji cha Roho Mtakatifu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

45 Wale Wayahudi waumini waliokuja pamoja na Petro kutoka Yopa walishangaa kuona kuwa Mungu aliwamiminia kipawa cha Roho Mtakatifu watu wa mataifa mengine pia;

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

45 Wale Wayahudi waumini waliokuja pamoja na Petro kutoka Yopa walishangaa kuona kuwa Mungu aliwamiminia kipawa cha Roho Mtakatifu watu wa mataifa mengine pia;

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

45 Wale Wayahudi waumini waliokuja pamoja na Petro kutoka Yopa walishangaa kuona kuwa Mungu aliwamiminia kipawa cha Roho Mtakatifu watu wa mataifa mengine pia;

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

45 Wale waumini waliokuwa wametahiriwa waliokuja na Petro walishangaa kwa kuona kuwa kipawa cha Roho wa Mungu kimemwagwa juu ya watu wa Mataifa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

45 Wale wa tohara walioamini waliokuja na Petro walishangaa kwa kuona kuwa kipawa cha Roho wa Mwenyezi Mungu kimemwagwa juu ya watu wa Mataifa.

Tazama sura Nakili




Matendo 10:45
12 Marejeleo ya Msalaba  

Akasema, Ingieni; akawakaribisha. Hatta siku ya pili, Petro akatoka pamoja nao, na baadhi ya ndugu waliokaa Yoppa wakafuatana nae.


Na Petro alipopanda kwenda Yerusalemi, wale walio wa Tohara wakashindana nae, wakisema,


Uliingia kwa watu wasiotahiriwa ukala nao.


Bassi akiisha kupandishwa hatta mkono wa kuume wa Mungu, na kupokea kwa Baba ile ahadi ya Roho Mtakatifu amekimwaga kitu hiki mnachokiona sasa na kukisikia.


Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe killa mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.


na tumaini halitahayarishi, kwa maana pendo la Mungu limekwisha kumiminwa katika mioyo yetu na Roho Mtakatifu tuliyepcwa sisi.


Sisi tulio Wayahudi kwa asili, wala si wenye dhambi wa mataifa,


Kwa ajili ya hayo kumbukeni kwamba zamani, ninyi mlio watu wa mataifa kwa jinsi ya mwili, mnaoitwa jina lenu wasiotahiriwra na wale wanaoitwa jina lao waliotahiriwa, yaani tohara ya mwili kwa mikono:


Tufuate:

Matangazo


Matangazo