Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 10:38 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

38 khabari za Yesu wa Nazareti, jinsi Mungu alivyomtia mafuta kwa Roho Mtakatifu na uguvu: nae akatembea huko na huko, akitenda kazi njema na kuponya wote walioonewa na Shetani; kwa maana Mungu alikuwa pamoja nae.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

38 Mnamjua Yesu wa Nazareti na jinsi Mungu alivyomteua kwa kummiminia Roho Mtakatifu na nguvu. Mungu alikuwa pamoja naye; yeye alikwenda huko na huko akitenda mema na kuwaponya wote waliokuwa wamevamiwa na Ibilisi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

38 Mnamjua Yesu wa Nazareti na jinsi Mungu alivyomteua kwa kummiminia Roho Mtakatifu na nguvu. Mungu alikuwa pamoja naye; yeye alikwenda huko na huko akitenda mema na kuwaponya wote waliokuwa wamevamiwa na Ibilisi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

38 Mnamjua Yesu wa Nazareti na jinsi Mungu alivyomteua kwa kummiminia Roho Mtakatifu na nguvu. Mungu alikuwa pamoja naye; yeye alikwenda huko na huko akitenda mema na kuwaponya wote waliokuwa wamevamiwa na Ibilisi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

38 Jinsi Mungu alivyompaka mafuta Isa Al-Nasiri katika Roho wa Mungu, na jinsi alivyoenda kila mahali akitenda mema na kuponya wote waliokuwa wameonewa na nguvu za ibilisi, kwa sababu Mungu alikuwa pamoja naye.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

38 Jinsi Mungu alivyomtia Isa Al-Nasiri mafuta katika Roho wa Mwenyezi Mungu na jinsi alivyokwenda huku na huko akitenda mema na kuponya wote waliokuwa wameonewa na nguvu za ibilisi, kwa sababu Mungu alikuwa pamoja naye.

Tazama sura Nakili




Matendo 10:38
40 Marejeleo ya Msalaba  

Nae Yesu akijua haya akatoka huko: makutano mengi wakamfuata; akawaponya wote,


Lakini mimi nikifukuza pepo kwa uweza wa Bobo ya Mungu, bassi ufalme wa Mungu umekujieni.


Akaondoka Yesu, akamfuata, pamoja na wanafunzi wake.


Na Yesu alikuwa akizunguka katika miji yote na vijiji, akifundisha katika masunagogi yao, akikhubiri injili ya ufalme, akiponya magonjwa yote na dhaifu zote katika watu.


Akastaajahu kwa sababu ya kutokuamini kwao. Akazungukazunguka katika vile vijiji, akifundisha.


Roho Mtakatifu akashuka juu yake kwa mfano wa kiwiliwili kama hua, sauti ikatoka mbinguni, Wewe ndiwe mwana wangu, mpendwa wangu, ndiwe unipendezae.


Roho ya Bwana ni juu yangu, Kwa sababu amenitia mafuia kuwakhubiri maskini khabari njema. Amenituma kuwaponya waliopondeka moyo, Kuwatangazia wafungwa kufunguliwa, na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha wa huru waliosetwa,


Alipokuwa katika kumwendea, yule pepo akambwaga akamraruararua. Yesu akamkaripia yule pepo mchafu, akamponya yule mtoto, akamrudishia baba yake.


Maana Mwana wa Adamu hakuja kuziangamiza roho za wana Adamu, bali kuziokoa. Wakaenda zao hatta mji mwingine.


Yesu akawajibu, Kazi njema nyingi nimewaonyesha zitokazo kwa Baba yangu: katika kazi hizo ni ipi mnayonipigia mawe?


Saa inakuja, naam, imekwisha kuja, mtatawanyika killa mmoja kwa mambo yake, mtaniacha mimi peke yangu; wala mimi si peke yangu, kwa kuwa Baba yupo pamoja nami.


huyu alikuja kwa Yesu usiku, akamwambia, Rabbi, twajua ya kuwa u mwalimu, umetoka kwa Mungu; kwa maana hakuna mtu awezae kuzifanya ishara hizi uzifanyazo wewe, illa Mungu awe pamoja nae.


Kwa kuwa yeye aliyetumwa na Mungu huyanena maneno ya Mungu: kwa sababu Mungu hampi Roho kwa kupima.


Msikitendee kazi chakula chenye kuharibika, bali chakula kidumucho hatta uzima wa milele, Mwana wa Adamu atakachowapeni: maana huyu ndiye aliyetiwa muhuri na Baba, yaani, Mungu.


jambo lile mmelijua, lililoenea katika Yahudi yote likianzia Galilaya, haada ya ubatizo alioukhubiri Yohana;


Enyi waume wa Israeli, sikieni maneno haya: Yesu wa Nazareti, mtu aliyedhihirishwa kwenu na Mungu kwa miujiza na ajabu na ishara, ambazo Mungu alizifanya kwa mkono wake kati yenu, kama ninyi wenyewe mnavyojua;


Umependa haki, umechukia maasi: kwa sababu hiyo Mungu, Mungu wako, amekutia mafuta, mafuta ya shangwe kupita wenzako.


Erevukeni, kesheni; kwa kuwa mshitaki wenu Shetani, kama simba angurumae, huzungukazunguka, akitafuta mtu amle;


Na ninyi mmepakwa mafuta nae aliye Mtakatifu na mnajua yote.


afanyae dhambi yu wa Shetani: kwa kuwa Shetani hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihiri, illi azivunje kazi za Shetani.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo