Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 10:35 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

35 bali katika killa taifa mtu amchae na kutenda haki hukuhaliwa nae.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

35 Mtu wa taifa lolote anayemcha Mungu na kutenda yaliyo sawa anapokelewa naye.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

35 Mtu wa taifa lolote anayemcha Mungu na kutenda yaliyo sawa anapokelewa naye.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

35 Mtu wa taifa lolote anayemcha Mungu na kutenda yaliyo sawa anapokelewa naye.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

35 lakini katika kila taifa, kila mtu amchaye na kutenda yaliyo haki hukubaliwa naye.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

35 lakini katika kila taifa, kila mtu amchaye na kutenda yaliyo haki hukubaliwa naye.

Tazama sura Nakili




Matendo 10:35
36 Marejeleo ya Msalaba  

Akaja kwake akasema, Salamu, uliyepewa neema, Bwana yu pamoja nawe.


mtu nitawa, mcha Mungu, yeye na nyumba yake yote, nae alikuwa akiwapa watu sadaka nyingi, na kumwomba Mungu siku zote.


Akawaambia, Mnajua ya kuwa si halali mtu aliye Myahudi aongee na mtu aliye wa taifa lingine wala kumwendea, hikini Mungu amenionya, nisimwite mtu awae yote mchafu wala najis.


wala hakufanya tofauti kati yetu sisi na wao, akiwasafisha mioyo yao kwa imani.


Bassi makanisa wakapata raha katika Yahudi yote na Galilaya na Samaria, wakajengewa, wakiendelea katika kicho cha Bwana, na faraja ya Roho Mtakatifu.


Kwa sababu sio waisikiao torati walio wenye haki mbele ya Mungu, bali ni wale waitendao torati watakaohesabiwa kuwa wenye haki.


Kwa maana watu wa mataifu wasio na sharia wafanyapo kwa tabia zao yaliyo ndani ya torati, bao wasio na sharia wamekuwa sharia kwa nafsi zao wenyewe:


ni haki ya Mungu, ipatwayo kwa kuwa na imani kwa Yesu Kristo, huja kwa watu wote, huwakalia watu wote waaminio.


Kwa maana katika Roho mmoja sisi sote tulibatizwa tukaingia katika mwili mmoja, ikiwa tu Wayahudi, au ikiwa tu Wayunani; ikiwa tu watumwa au ikiwa tu huru; nasi sote tulinyweshwa Roho mmoja.


BASSI, kwa kuwa tuna ahadi hizo, wapenzi, tujitakase nafsi zelu uchafu wote wa mwili na roho, tukitimiza utakatifu katika kumeha Mungu.


Hapana Myahudi wala Myunani. Hapana mtumwa wala huru. Hapana mtu mume wala mtu mke. Maana ninyi nyote ni mmoja katika Kristo Yesu.


illi usifiwe utukufu wa neema yake, aliyotukarimu katika mpendwa wake:


mkitumikiana katika khofu ya Kristo.


Maana sisi tu tohara, tumwabuduo Muugu kwa Roho, na kujisifu katika Kristo Yesu, wala hatuutumainii mwili. Walakini mimi ningeweza kuutumainia mwili.


iliyofika kwenu, kama ilivyo katika ulimwengu wote, ikizaa matunda na kukua, kama na inavyokua kwenu, tangu siku mliposikia nikaifahamu sana neema ya Mungu katika kweli;


Hapo hapana Myunani wala Myahudi, kutahiriwa wala kutokutahiriwa, mshenzi wala Mskuthi, mtumwa wala mungwana, bali Kristo ni yote, na katika wote.


Kama mkijua ya kuwa yeye ni mwenye haki, jueni ya kuwa killa atendae haki amezaliwa nae.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo