Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 10:3 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

3 Akaona katika njozi wazi wazi, panapo saa tissa ya mchana, malaika wa Mungu akimjia na kumwambia, Kornelio!

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 Yapata saa tisa alasiri, aliona dhahiri katika maono malaika wa Mungu akiingia ndani na kumwambia, “Kornelio!”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

3 Yapata saa tisa alasiri, aliona dhahiri katika maono malaika wa Mungu akiingia ndani na kumwambia, “Kornelio!”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 Yapata saa tisa alasiri, aliona dhahiri katika maono malaika wa Mungu akiingia ndani na kumwambia, “Kornelio!”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 Siku moja alasiri, yapata saa tisa, aliona maono waziwazi, malaika wa Mungu akimjia na kumwambia, “Kornelio!”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

3 Siku moja alasiri, yapata saa tisa, aliona maono waziwazi, malaika wa Mungu akimjia na kumwambia, “Kornelio!”

Tazama sura Nakili




Matendo 10:3
23 Marejeleo ya Msalaba  

Na kama saa tissa, Yesu akapaaza sauti yake kwa nguvu akinena, Eli, Eli, lama sabakhthani? maana yake, Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?


Akatokewa na Malaika wa Bwana, amesimama upande wa kuume wa madhbahu ya kufukizia.


Ghafula hiyo walikuwapo pamoja na yule malaika wengi wa jeshi la mbinguni, wakimsifu Mungu, wakisema,


Hatta Petro alipokuwa akiona mashaka ndani ya nafsi yake, maana yake nini maono hayo aliyoyaona, wale watu waliotumwa na Kornelio, wakiislia kuiulizia nyumba ya Simon, wakasimama mbele ya mlango,


Na Petro alikuwa akiyafikiri yale maono. Roho akamwambia, Wako watu watatu wanakutaka.


Kornelio akanena, Leo ni siku ya nne tangu nilijiokuwa nikifunga hatta saa hii: na saa tissa nalikuwa nikisali nyumbani mwangu: kumbe! mtu amesimama mbele yangu, mwenye nguo zingʼaazo, akasema,


Hatta siku ya pili, walipokuwa wakisafiri na kuukaribia mji, Petro alipanda juu darini, kwenda kuomba, panapo saa sita ya mchana:


akatueleza jinsi alivyomwona malaika aliyesimama nyumbani mwake na kumwambia, Tuma watu kwenda Yoppa ukamwite Simon, aitwae Petro


Kwa maana usiku huu wa leo malaika wa Mungu yule ambae mimi ni mtu wake, na udiye nimtumikiae, alisimama karibu nami akaniambia,


BASSI Petro na Yohana walikuwa wakipanda pamoja kwenda hekaluni, saa ya kusali, saa tissa.


lakini malaika wa Bwana akafungua milango ya gereza usiku, akawatoa, akasema,


Bassi palikuwapo mwanafunzi Dameski, jina lake Anania. Bwana akamwambia katika njozi, Anania. Akasema, Mimi hapa, Bwana.


Akaanguka chini, akasikia sauti ikimwambia, Saul, Saul, mbona wanifukuza?


Hawo wote si roho zitumikazo, wakitumwa kuwakhudumu wale watakaourithi wokofu?


amefanyika bora sana kupita malaika, kwa kadiri jina alilolirithi lilivyo tukufu kuliko wao.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo