Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 10:23 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

23 Akasema, Ingieni; akawakaribisha. Hatta siku ya pili, Petro akatoka pamoja nao, na baadhi ya ndugu waliokaa Yoppa wakafuatana nae.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

23 Petro akawakaribisha ndani, akawapa mahali pa kulala usiku ule. Kesho yake, Petro alianza safari pamoja nao, na baadhi ya ndugu wa huko Yopa walifuatana naye.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

23 Petro akawakaribisha ndani, akawapa mahali pa kulala usiku ule. Kesho yake, Petro alianza safari pamoja nao, na baadhi ya ndugu wa huko Yopa walifuatana naye.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

23 Petro akawakaribisha ndani, akawapa mahali pa kulala usiku ule. Kesho yake, Petro alianza safari pamoja nao, na baadhi ya ndugu wa huko Yopa walifuatana naye.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

23 Basi Petro akawakaribisha ndani wawe wageni wake. Kesho yake akaondoka pamoja nao, na baadhi ya ndugu kutoka Yafa wakafuatana naye.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

23 Basi Petro akawakaribisha wakafuatana naye ndani, akawapa pa kulala. Kesho yake akaondoka pamoja nao, na baadhi ya ndugu kutoka Yafa wakafuatana naye.

Tazama sura Nakili




Matendo 10:23
16 Marejeleo ya Msalaba  

Siku zile akasimama Petro kati ya wanafunzi, akasema (jumla ya majina ilipata mia na ishirini),


Kwa sababu hiyo naiikuja nilipoitwa nisikatae; hassi nauliza, ni neno gani mliloniitia?


Marra nikatuma watu kwako, nawe umefanya vyema kuja. Bassi sasa sisi sote tupo hapa mbele za Mungu, tupate kuyasikiliza maneno yote uliyoamriwa na Mungu.


Na wale waliotahiriwa walioamini, wakashangaa, watu wote waliokuja pamoja na Petro, kwa sababu mataifa nao wameshukiwa kipaji cha Roho Mtakatifu.


Roho akaniambia nifuatane nao, nisione mashaka. Ndugu hawa sita nao wakaenda pamoja nami, tukaingia katika nyumba ya mtu yule:


Na kutoka huko ndugu, waliposikia khabari zetu, wakaja kutulaki mpaka Appiiforo na Trestaberne. Paolo alipowaona akamshukuru Mungu, akachangaʼmka.


Na mwanafunzi mmoja alikuwako Yoppa, jina lake Tabitha, (tafsiri yake ni paa:) mwanamke huyu alikuwa amejaa matendo mema na sadaka alizozitoa.


Na kwa kuwa Ludda ulikuwa karibu na Yoppa, nao wamesikia ya kwamha Petro yuko huko, wakatuma watu wawili kwake, kumsihi asikawie kuja kwao.


Ikajulikana katika Yoppa, katika mji mzima, watu wengi wakamwamini Bwana.


tukitangulia kufikiri yaliyo mema, si mbele ya Bwana tu, bali na mbele ya wana Adamu.


Msisahau kuwafadhilia wageni; maana kwa njia hii wengine wamewakaribisha malaika pasipo kujua.


mwe wakaribishaji ninyi kwa ninyi, pasipo kunnngʼunika;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo