Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 10:22 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

22 Wakasema, Kornelio akida, mtu mwenye haki, mcha Mungu, aliye na sifa njema kwa taifa lote la Wayahudi, alionywa na malaika mtakatifu kutuma watu kwako, uende nyumbani kwake, apate kusikiliza maneno yako.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

22 Wao wakamjibu, “Jemadari Kornelio ambaye ni mtu mwema, mcha Mungu na mwenye kuheshimika mbele ya Wayahudi wote, ametutuma. Aliambiwa na malaika mtakatifu akualike nyumbani kwake ili asikilize chochote ulicho nacho cha kusema.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

22 Wao wakamjibu, “Jemadari Kornelio ambaye ni mtu mwema, mcha Mungu na mwenye kuheshimika mbele ya Wayahudi wote, ametutuma. Aliambiwa na malaika mtakatifu akualike nyumbani kwake ili asikilize chochote ulicho nacho cha kusema.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

22 Wao wakamjibu, “Jemadari Kornelio ambaye ni mtu mwema, mcha Mungu na mwenye kuheshimika mbele ya Wayahudi wote, ametutuma. Aliambiwa na malaika mtakatifu akualike nyumbani kwake ili asikilize chochote ulicho nacho cha kusema.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

22 Wale watu wakamjibu, “Tumetumwa na Kornelio yule jemadari. Yeye ni mtu mwema anayemcha Mungu, na anaheshimiwa na Wayahudi wote. Yeye ameagizwa na malaika mtakatifu akukaribishe nyumbani mwake, ili asikilize maneno utakayomwambia.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

22 Wale watu wakamjibu, “Tumetumwa na Kornelio yule jemadari. Yeye ni mtu mwema anayemcha Mungu, na anaheshimiwa na Wayahudi wote. Yeye ameagizwa na malaika mtakatifu akukaribishe nyumbani kwake, ili asikilize maneno utakayomwambia.”

Tazama sura Nakili




Matendo 10:22
36 Marejeleo ya Msalaba  

Nae Yusuf, mumewe, kwa kuwa mtu wa haki, asitake kumwaibisha, aliazimu kumwacha kwa siri.


Nao wakiisha kuonywa katika ndoto wasimrudie Herode, wakaenda zao kwao kwa njia nyingine.


Maana Herode alimwogopa Yohana: hatta akimjua kuwa ni mtu wa haki, mtakatifu, akamhami, na alipokwisha kumsikiliza alifanya mambo mengi: nae alikuwa akimsikiliza kwa furaha.


Maana killa mtu atakaenionea haya mimi, na maneno yangu, katika kizazi hiki cha zina na dhambi, Mwana wa Adamu atamwonea haya yeye atakapokuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika watakatifu.


Bassi kulikuwako mtu katika Yerusalemi, jina lake Sumeon; na yule mtu mwenye haki, mtawa, akitazamia faraja ya Israeli: na Roho Mtakatifu alikuwa pamoja nae.


Akatoka mtu, jina lake Yusuf, nae ni mtu wa baraza yao, mtu mwema, mwenye haki


Kwa sababu killa mtu atakaenionea haya mimi na maneno yangu, Mwana wa Adamu atamwonea haya huyo atakapokuja katika utukufu wake, na wa Baba yake, na wa malaika watakatifu.


Amin, amin, nawaambieni, Yeye ampokeae ye yote nimpelekae, anipokea mimi; nae anipokeae mimi, ampokea yeye aliyenipeleka.


Wala si hao tu ninaowaombea, bali na wao walakaoniammi kwa sababu ya neno lao.


kwa kuwa maneno uliyonipa nimewapa wao; wakavapokea, wakajua hakika ya kuwa nalitoka kwako, wakaamini ya kwamba ndiwe uliyenituma.


Amin, amin, nawaambieni, Alisikiae neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka ana uzima wa milele, wala hafiki hukumuni, bali amepita toka mauti hatta uzima.


Roho ndiyo itiayo uzima; mwili haufai kitu; maneno ninayowaambieni ni roho, tena ni uzima.


Bassi Simon Petro akamjibu, Bwana! twende kwa nani? Wewe una maneno ya uzima wa milele.


mtu nitawa, mcha Mungu, yeye na nyumba yake yote, nae alikuwa akiwapa watu sadaka nyingi, na kumwomba Mungu siku zote.


Petro akawashukia wale watu waliotumwa kwake na Kornelio, akanena, Mimi ndiye mnaemtaka. Mmekuja kwa sababu gani?


Kornelio akanena, Leo ni siku ya nne tangu nilijiokuwa nikifunga hatta saa hii: na saa tissa nalikuwa nikisali nyumbani mwangu: kumbe! mtu amesimama mbele yangu, mwenye nguo zingʼaazo, akasema,


Marra nikatuma watu kwako, nawe umefanya vyema kuja. Bassi sasa sisi sote tupo hapa mbele za Mungu, tupate kuyasikiliza maneno yote uliyoamriwa na Mungu.


Yeye ni mgeni wa mtu mmoja, jina lake Simon, mtengenezaji wa ngozi; nyumba yake iko pwani; atakuambia yakupasayo kutenda.


atakaekuambia maneno ambayo utaokolewa nayo, wewe na nyumba yako yote.


Bassi mtu mmoja, Anania, mcha Mungu kwa kuifuata sharia, aliyeshuhudiwa na Wayahudi wote waliokaa huko, akanijia, akasimama karibu nami, akaniambia, Ndugu, Saul, uone.


Nina tumaini kwa Mungu, na hatta hao nao wanalitazamia, ya kwamba kutakuwa ufufuo wa wafu wenye haki na wasio haki pia.


Bassi ndugu, chagueni watu saba miongoni mwenu, walioshuhudiwa kuwa wema, illi tuwaweke juu ya jambo hili:


Kwa maana haki ya Mungu inadhihirishwa ndani yake, toka imani hatta imani; kama ilivyoandikwa, Mwenye haki ataishi kwa imani.


Lakini vyote pia vyatokana na Mungu, aliyetupatanisha sisi na nafsi yake kwa Kristo, nae alitupa khuduma ya upatauisho;


Imempasa tena kushuhudiwa mazuri na watu walio nje; asitumbukie katika lawama na mtego wa Shetani.


Lakini mwenye haki ataishi kwa imani; nae akisitasita, roho yangu haina furaha nae.


Maana kwa hiyo wazee wetu walishuhudiwa.


na kanisa la wazaliwa wa kwanza walioandikwa mbinguni, na Mungu mwamuzi wa watu wote, na roho za watu wenye haki waliokamilika,


mpate kuyakumbuka maneno yaliyonenwa zamani na manabii watakatifu, na ile amri ya Bwana Mwokozi iliyoletwa na mitume wake.


Demetrio ameshuhudiwa na watu wote, tena na ile kweli yenyewe. Na sisi pia twashuhudu, nawe wajua ya kwamba ushuhuda wetu ni kweli.


yeye nae atakunywa mvinyo ya hasira ya Mungu iliyotengenezwa pasipo kuchanganywa na maji katika kikombe cha ghadhabu yake, nae ataumwa kwa moto na kiberiti mbele ya malaika walakalifu na mbele za Mwana kondoo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo