Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 10:2 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

2 mtu nitawa, mcha Mungu, yeye na nyumba yake yote, nae alikuwa akiwapa watu sadaka nyingi, na kumwomba Mungu siku zote.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 Alikuwa mtu mwema; naye pamoja na jamaa yake yote walimcha Mungu; alikuwa anafanya mengi kusaidia maskini wa Kiyahudi na alikuwa anasali daima.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

2 Alikuwa mtu mwema; naye pamoja na jamaa yake yote walimcha Mungu; alikuwa anafanya mengi kusaidia maskini wa Kiyahudi na alikuwa anasali daima.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 Alikuwa mtu mwema; naye pamoja na jamaa yake yote walimcha Mungu; alikuwa anafanya mengi kusaidia maskini wa Kiyahudi na alikuwa anasali daima.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 Yeye na jamaa yake yote walikuwa wacha Mungu; alitoa kwa ukarimu kwa wale walio na mahitaji na kumwomba Mungu mara kwa mara.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 Yeye alikuwa mcha Mungu pamoja na wote wa nyumbani mwake. Aliwapa watu sadaka nyingi na kumwomba Mwenyezi Mungu daima.

Tazama sura Nakili




Matendo 10:2
51 Marejeleo ya Msalaba  

Vilevile na yule mwenye mbili, yeye nae akachuma nyingine mbili faida.


AKAWAAMBIA na mfano ya kama imewapasa kumwomba Mungu siku zote wala wasikate tamaa,


Bassi kulikuwako mtu katika Yerusalemi, jina lake Sumeon; na yule mtu mwenye haki, mtawa, akitazamia faraja ya Israeli: na Roho Mtakatifu alikuwa pamoja nae.


Wakasema, Kornelio akida, mtu mwenye haki, mcha Mungu, aliye na sifa njema kwa taifa lote la Wayahudi, alionywa na malaika mtakatifu kutuma watu kwako, uende nyumbani kwake, apate kusikiliza maneno yako.


Kornelio, maombi yako yamesikiwa, na sadaka zako zinakumbukwa mbele za Mungu.


bali katika killa taifa mtu amchae na kutenda haki hukuhaliwa nae.


Akamtazama sana, akaogopa akasema, Kuna nini, Bwana? Akamwambia, Maombi yako na sadaka zako zimefika juu na kuwa ukumbusho mbele za Mungu.


Na yule malaika aliyesema nae akiisha kuondoka, Kornelio akaita watumishi wawili wa nyumba yake, na askari mmoja, mtu mtawa, katika wale waliomkhudumia daima:


atakaekuambia maneno ambayo utaokolewa nayo, wewe na nyumba yako yote.


Paolo akasimama, akawtipungia mkono, akanena, Enyi wanme wa Israeli, na ninyi mnaomcha Mungu, sikilizeni.


Ndugu zangu, wana wa ukoo wa Ibrahimu, nao miongoni mwenu mnaomcha Mungu, kwenu ninyi neno la wokofu huu limepelekwa.


Lakini Wayahudi wakawafitinisha wanawake watawa na watu wenye cheo na wakuu wa mji, wakawataharakisha watu wawaudhi Paolo na Barnaba; wakawatoa katika mipaka yao.


Na Krispo, mkuu wa sunagogi, akamwamini Bwana pamoja na nyumba yake yote. Wakorintho wengi wakasikia, wakaamini, wakabatizwa.


Na walikuwako Yerusalemi Wayahudi wakikaa, watu watawa, watu wa killa taifa chini ya uwingu.


Bassi mtu mmoja, Anania, mcha Mungu kwa kuifuata sharia, aliyeshuhudiwa na Wayahudi wote waliokaa huko, akanijia, akasimama karibu nami, akaniambia, Ndugu, Saul, uone.


Watu watawa wakamzika Stefano, wakamfanyia maombolezo mengi.


Bwana akamwambia, Simama, enenda zako katika njia iitwayo Sawa, ukatafute ndani ya nyumba ya Yuda mtu jina lake Saul, wa Tarso: maana yuko anasali:


Bassi makanisa wakapata raha katika Yahudi yote na Galilaya na Samaria, wakajengewa, wakiendelea katika kicho cha Bwana, na faraja ya Roho Mtakatifu.


Na mwanafunzi mmoja alikuwako Yoppa, jina lake Tabitha, (tafsiri yake ni paa:) mwanamke huyu alikuwa amejaa matendo mema na sadaka alizozitoa.


Dumuni sana katika kuomba, mkikesha katika kuomba huku na shukrani,


Lakini mtu wa kwemi akipungukiwa hekima, aombe dua kwa Mungu, awapae wote kwa ukarimu, wala hakemei; nae atapewa.


Ni nani asiyekucha, Bwana, na kulitukuza jina lako? kwa kuwa wewe peke yako Mtakatifu: kwa maana mataifa yote watakuja na kusujudu mbele yako; kwa kuwa matendo yako ya haki yamekwisha kufunuliwa.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo