Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 10:14 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

14 Petro akasema, Hasha, Bwana, kwa maana sijala kamwe kitu kilicho kichafu au najis.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 Petro akajibu, “La, Bwana; mimi sijaonja kamwe chochote ambacho ni najisi au kichafu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

14 Petro akajibu, “La, Bwana; mimi sijaonja kamwe chochote ambacho ni najisi au kichafu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 Petro akajibu, “La, Bwana; mimi sijaonja kamwe chochote ambacho ni najisi au kichafu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 Petro akajibu, “La hasha, Bwana! Sijawahi kamwe kula kitu chochote kilicho najisi.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 Petro akajibu, “La hasha, Bwana Mwenyezi! Sijawahi kamwe kula kitu chochote kilicho najisi.”

Tazama sura Nakili




Matendo 10:14
19 Marejeleo ya Msalaba  

Sicho kiingiacho kinywani kimtiacho najis mwana Adamu; bali kitokacho kinywani ndicho kimtiacho najis mwana Adamu.


Petro akamchukua, akaanza kumkemea, akinena, Hasha, Bwana, haya hayatakupata.


Lakini wale wenye busara wakawajibu, wakinena, Labuda hayatatutosha sisi na ninyi; afadhali shikeni njia kwenda kwao wauzao, mkanunue wenyewe.


Akaja mwenye ukoma akamsujudu, akinena, Bwana, ukitaka, waweza kunitakasa.


wakaona baadhi ya wanafunzi wake wakila vyakula kwa mikono najis, yaani, yasiyonawiwa, wakawalaumu.


Akajibu mamae, akasema, Sivyo, lakini atakwitwa Yohana.


Yule mwanamke akamwambia, Bwana, huna kitu cha kutekea na kisima kinakwenda chini sana; bassi, umeyapata wapi haya maji yaliyo hayi?


Sauti ikamjia, Ondoka, Petro, ukachinje ule.


Akawaambia, Mnajua ya kuwa si halali mtu aliye Myahudi aongee na mtu aliye wa taifa lingine wala kumwendea, hikini Mungu amenionya, nisimwite mtu awae yote mchafu wala najis.


Nikajibu Wewe nani Bwana? Akaniambia, Mimi ni Yesu Mnazareti, ambae wewe unaniudhi.


Akasema, U nani Bwana? Akasema, Mimi ndimi Yesu unaeniudhi wewe.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo