Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 10:11 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

11 na chombo kikimshukia kama nguo kubwa, kinatelemshwa kwa pembe zake nne hatta inchi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 Aliona mbingu zimefunguliwa na kitu kama shuka kubwa inateremshwa chini ikiwa imeshikwa pembe zake nne.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 Aliona mbingu zimefunguliwa na kitu kama shuka kubwa inateremshwa chini ikiwa imeshikwa pembe zake nne.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 Aliona mbingu zimefunguliwa na kitu kama shuka kubwa inateremshwa chini ikiwa imeshikwa pembe zake nne.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 Akaona mbingu zimefunguka na kitu kama kitambaa kikubwa kikishushwa duniani kwa ncha zake nne.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 Akaona mbingu zimefunguka na kitu kama nguo kubwa kikishushwa duniani kwa ncha zake nne.

Tazama sura Nakili




Matendo 10:11
28 Marejeleo ya Msalaba  

Nami nawaambieni, ya kwamba wengi watakuja kutoka mashariki na magbaribi, wataketi pamoja na Ibrabimu, na Isaak, na Yakob katika ufalme wa mbinguni;


Na watu wote walipokwisha kubatizwa, na Yesu nae akiisha kubatizwa, na akisali, mbingu zilifunuka.


Akamwambia, Amin, amin, nakuambieni, Tangu sasa mtaziona mbingu zimefunguka, na malaika wa Mungu wakipanda, wakishuka juu ya Mwana wa Adamu.


wala si kwa ajili ya taifa lile tu, lakini pamoja na haya awakusanye watoto wa Mungu waliotawanyika wawe wamoja.


Nami nikiinuliwa juu ya inchi nitavuta wote kwangu.


Ndani yake aina zote za nyama zenye miguu mine, na nyama za mwituni, nazo zitambaazo, na ndege za anga.


Nalikuwa katika mji wa Yoppa, nikiomba, roho yangu ikazimia, nikaona maono; chombo kama nguo kubwa kikishuka, kinashushwa kutoka mbinguni kwa pembe zake nne, kikanifikilia.


Akasema, Tazama! naona mbingu zimefunuliwa, na Mwana wa Adamu amesimama mkono wa Mungu.


kwa maana siionci haya Injili; kwa sababu ni uweza wa Mungu uuletao wokofu, kwa killa aaminiye, kwa Myahudi kwanza, hatta kwa Myunani pia.


ambao ni Waisraeli, wenye kufanywa wana, wenye utukufu na maagano, wenye kupewa torati na ibada ya Mungu na ahadi zake; ambao mababu ni wao,


Sisi tulio Wayahudi kwa asili, wala si wenye dhambi wa mataifa,


Hapana Myahudi wala Myunani. Hapana mtumwa wala huru. Hapana mtu mume wala mtu mke. Maana ninyi nyote ni mmoja katika Kristo Yesu.


ya kwamba wakati mkamilifu utakapowadia atajumlisha vitu vyote viwe umoja katika Kristo, vitu vilivyo mbinguni, navyo vilivyo duniani, katika yeye huyu:


ya kwamba mataifa ni warithi pamoja nasi wa urithi mmoja, na wa mwili mmoja, na washiriki pamoja nasi ahadi yake iliyo katika Kristo kwa njia ya injili;


Hapo hapana Myunani wala Myahudi, kutahiriwa wala kutokutahiriwa, mshenzi wala Mskuthi, mtumwa wala mungwana, bali Kristo ni yote, na katika wote.


Hekalu ya Mungu ikafunguliwa mbinguni na sanduku la agano likaonekana ndani ya hekalu yake. Kukawa umeme, na sauti, na radi, na tetemeko, na mvua ya mawe uyingi sana.


Nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama farasi mweupe, nae aliyempanda, aitwae Mwaminifu na wa kweli, nae kwa haki ahukumu na kufanya vita.


BAADA ya haya naliona, na tazama mlango ukafunguka mbinguni, na sauti ya kwanza niliyoisikia kama sauti ya baragumu ikinena nami, ikisema, Panda hatta huku, nami nitakuonyesha mambo ambayo hayana buddi kuwa baada ya bayo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo