Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 1:8 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

8 Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemi, na katika Yahudi yote, na Samaria, na hatta mwisho wa inchi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

8 Lakini wakati Roho Mtakatifu atakapowashukieni nyinyi, mtapokea nguvu na mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, katika nchi yote ya Yudea na Samaria, na hata miisho ya dunia.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

8 Lakini wakati Roho Mtakatifu atakapowashukieni nyinyi, mtapokea nguvu na mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, katika nchi yote ya Yudea na Samaria, na hata miisho ya dunia.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

8 Lakini wakati Roho Mtakatifu atakapowashukieni nyinyi, mtapokea nguvu na mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, katika nchi yote ya Yudea na Samaria, na hata miisho ya dunia.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

8 Lakini mtapokea nguvu, Roho wa Mungu akiwajilia juu yenu, nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na Yudea yote, na Samaria, na miisho ya dunia.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

8 Lakini mtapokea nguvu akiisha kuwajilia juu yenu Roho wa Mwenyezi Mungu, nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, Uyahudi kote na Samaria, hadi miisho ya dunia.”

Tazama sura Nakili




Matendo 1:8
34 Marejeleo ya Msalaba  

Na injili hii ya ufalme itakhubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; ndipo ule mwisho utakapokuja.


Bassi, enendeni, kawafanyeni mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;


Akawaambia, Enendem nlimwenguni mwote, mkaikhubiri injili kwa killa kiumbe.


Malaika akajibu, akamwambia, Roho Mtakatifu atakujia, na nguvu zake Aliye juu zitakutilia kivuli: kwa biyo kitakachozaliwa kitakwitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu.


Tazameni, nawapeni mamlaka va kuwakanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hapana kitu kitakachowadhuru ninyi kamwe.


Wakamshurutisha, wakisema, Kaa pamoja nasi, kwa maana kumekuchwa, na mchana unakwisha sasa. Akaingia kukaa nao.


Na ninyi pia mnashunudu, kwa kuwa tangu mwanzo mmekuwa pamoja nami.


akianza tangu ubatizo wa Yohana, hatta siku ile alipochukuliwa kwetu kwenda juu, lazima mmoja wao afanywe shahidi wa kufufuka kwake pamoja nasi.


ya kwamba Yohana alibatiza kwa maji, bali ninyi mtabatizwa katika Roho Mtakatifu baada ya siku hizi si nyingi.


akaonwa siku nyingi nao waliopanda nae kutoka Galilaya hatta Yerusalemi, na hao ndio walio sasa mashahidi wake mbele va watu.


Yesu huyo Mungu alimfufua, na sisi sote tu mashahidi wake.


Kwa maana utakuwa shahidi wake kwa watu wote, wa mambo hayo uliyoyaona na kuyasikia.


mkamwua yule Mkuu wa uzima, ambae Mungu amemfufua: na sisi tu mashahidi wake.


Na mitume wakatoa ushuhuda wa kufufuka kwake Yesu kwa uguvu nyingi. Neema nyingi ikawa juu yao wote.


Na sisi tu mashahidi wa mambo haya, pamoja na Roho Mtakatifu ambae Mungu amewapa wote wamtiio.


Na Stefano, akijaa imani na uwezo, alikuwa akifanya maajabu na ishara kubwa katika watu.


NA Saul alikuwa akiona vema auawe. Siku ile kukatukia adha nyingi juu ya kanisa lililokuwa katika Yerusalemi: wote wakatawanyika katika inchi ya Yahudi na Samaria, illa mitume.


Lakini nasema, Wao hawakusikia? Naam, wamesikia, Sauti yao imetoka ikaenea katika inchi yote, Na maneno yao hatta miisho ya ulimwengu.


katika nguvu za Roho Mtakatifu; hatta ikawa tangu Yerusalemi, na kando kando yake, hatta Illuriko nimekwisha kuikhubiri Injili ya Kristo kwa utimilifu,


mkidumu tu katika imani, mmewekwa juu ya misingi, mkawa imara; msipogeuzwa na kuliacha tumaini la Injili mliyosikia khabari zake, iliyokhubiriwa katika viumbe vyote vilivyo chini ya mbingu; ambayo mimi Paolo nalikuwa mkhudumu wake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo