Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 1:7 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

7 Akawaambia, Si kazi yenu kujua nyakati wala majira, Baba aliyoyaweka katika mamlaka yake mwenyewe.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

7 Lakini Yesu akawaambia, “Nyakati na majira ya mambo hayo viko chini ya mamlaka ya Baba yangu, wala si shauri lenu kujua yatakuwa lini.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

7 Lakini Yesu akawaambia, “Nyakati na majira ya mambo hayo viko chini ya mamlaka ya Baba yangu, wala si shauri lenu kujua yatakuwa lini.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

7 Lakini Yesu akawaambia, “Nyakati na majira ya mambo hayo viko chini ya mamlaka ya Baba yangu, wala si shauri lenu kujua yatakuwa lini.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

7 Isa akawaambia, “Sio wajibu wenu kujua nyakati au majira ambayo Baba ameyaweka kwa mamlaka yake mwenyewe.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

7 Isa akawaambia, “Si juu yenu kujua nyakati na majira ambayo Baba ameyaweka katika mamlaka yake mwenyewe.

Tazama sura Nakili




Matendo 1:7
13 Marejeleo ya Msalaba  

Akawaambia, Hakika mtakinywea kikombe changu, na mtabatizwa ubatizo nibatizwao mimi; lakini kuketi mkono wangu wa kuume na mkono wangu wa kushoto, sina amri niwapeni, bali watapewa waliowekewa tayari na Baba yangu.


Na khabari ya siku ile na saa ile hakuna ajuae, hatta malaika walio mbinguni, illa, Baba yangu peke yake.


bali khabari ya kuketi mkono wangu wa kuume na mkono wangu wa kushoto sina amri kuwapeni, illa wao watapewa waliowekewa tayari.


Lakini khabari ya siku ile na saa ile hakuna aijuae, hatta malaika walio mbinguni, wala Mwana, illa Baba.


Nao wataanguka kwa ukali wa upanga, watachukuliwa mateka mpaka mataifa yote: nao Yerusalemi utakanyagwa na mataifa, hatta majira ya mataifa yatakapotimia.


Nae alifanya killa taifa ya wana Adamu kuwa wa damu moja, wakae juu ya uso wa inchi yote, akiisha kuwaandikia nyakati alizowaamuru tangu zamani, na mipaka ya makazi yao;


ya kwamba wakati mkamilifu utakapowadia atajumlisha vitu vyote viwe umoja katika Kristo, vitu vilivyo mbinguni, navyo vilivyo duniani, katika yeye huyu:


ambako katika nyakati zake mwenyewe ataonyesha yeye mwenye uweza wote, Mfalme wa Wafalme, Bwana wa Mabwana,


LAKINI ujue neno hili, ya kuwa siku za mwisho zitakuwa nyakati za khatari.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo