Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 1:5 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

5 ya kwamba Yohana alibatiza kwa maji, bali ninyi mtabatizwa katika Roho Mtakatifu baada ya siku hizi si nyingi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 Kwani Yohane alibatiza kwa maji, lakini baada ya siku chache, nyinyi mtabatizwa kwa Roho Mtakatifu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

5 Kwani Yohane alibatiza kwa maji, lakini baada ya siku chache, nyinyi mtabatizwa kwa Roho Mtakatifu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 Kwani Yohane alibatiza kwa maji, lakini baada ya siku chache, nyinyi mtabatizwa kwa Roho Mtakatifu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 Yahya aliwabatiza kwa maji, lakini baada ya siku chache mtabatizwa kwa Roho wa Mungu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 Yahya aliwabatiza kwa maji, lakini baada ya siku chache mtabatizwa kwa Roho wa Mwenyezi Mungu.”

Tazama sura Nakili




Matendo 1:5
16 Marejeleo ya Msalaba  

Mimi nawabatizeni katika maji mpate kutubu: bali yeye ajae nyuma yangu ni hodari kuliko mimi, wala sistahili hatta kuchukua viatu vyake; yeye atawabatizeni kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.


wakabatizwa nae mtoni Yordani, wakiziungama dhambi zao.


Mimi naliwabatizeni kwa maji; bali yeye atawabalizeni kwa Roho Mtakatifu.


Yohana akajibu, akawaambia wote, Mimi nawabatiza kwa maji, lakini yuaja aliye hodari kuliko mimi, ambae kwamba mimi sistahili kumfungulia ukanda wa viatu vyake; yeye atawabatizeni kwa Roho Mtakatifu na kwa moto:


Yohana akawajibu akanena, Mimi nabatiza kwa maji: kati mwenu amesimama msiyemjua ninyi.


Nami sikumjua: lakini kusudi adhibirishwe kwa Israeli ndio maana nalikuja nikibatiza kwa maji.


Nami sikumjua, lakini yeye aliyenipeleka kubatiza kwa maji, huyu aliniambia, Yeye ambae utakaemwona Roho akishuka na kukaa juu yake, huyu ndiye abatizae kwa Roho Mtakatifu.


Na wale waliotahiriwa walioamini, wakashangaa, watu wote waliokuja pamoja na Petro, kwa sababu mataifa nao wameshukiwa kipaji cha Roho Mtakatifu.


Paolo akasema, Yohana alibatiza kwa ubatizo wa toba, akiwaambia watu wamwamini yeye atakaekuja nyuma yake, yaani Kristo Yesu.


Kwa maana katika Roho mmoja sisi sote tulibatizwa tukaingia katika mwili mmoja, ikiwa tu Wayahudi, au ikiwa tu Wayunani; ikiwa tu watumwa au ikiwa tu huru; nasi sote tulinyweshwa Roho mmoja.


alituokoa, si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda, bali kwa rehema yake, kwa josho la kuzaliwa kwa pili, na kufanywa upya na Roho Mtakatifu,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo