Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 1:15 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

15 Siku zile akasimama Petro kati ya wanafunzi, akasema (jumla ya majina ilipata mia na ishirini),

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

15 Siku moja baadaye, Petro alisimama kati ya wale ndugu waumini ambao walikuwa wamekusanyika, wote jumla watu 120,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

15 Siku moja baadaye, Petro alisimama kati ya wale ndugu waumini ambao walikuwa wamekusanyika, wote jumla watu 120,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

15 Siku moja baadaye, Petro alisimama kati ya wale ndugu waumini ambao walikuwa wamekusanyika, wote jumla watu 120,

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

15 Katika siku hizo Petro akasimama katikati ya waumini (jumla yao walikuwa watu wapatao mia moja na ishirini), akasema,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

15 Katika siku hizo Petro akasimama katikati ya waumini (jumla yao wote walikuwa watu wapatao 120), akasema,

Tazama sura Nakili




Matendo 1:15
31 Marejeleo ya Msalaba  

Akawatolea mfano mwingine, akisema, Ufalme wa mbinguni umefanana na punje ya kharadali, aliyotwati mtu akaipanda katika shamba lake;


lakini nimekuombea, illi imani yako isipunguke; nawe uongokapo, wathubutishe ndugu zako.


Amin, amin, nawaambieni, Aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi na yeye atazifanya; atafanya na kubwa kuliko hizi, kwa kuwa nashika njia kwenda kwa Baba.


Bassi neno hili lilienea katika ndugu kwamba mwanafunzi yule hafi: walakini Yesu hakumwambia, Hafi; bali, Nikitaka akae hatta nijapo imekukhusu nini?


Akasema, Ingieni; akawakaribisha. Hatta siku ya pili, Petro akatoka pamoja nao, na baadhi ya ndugu waliokaa Yoppa wakafuatana nae.


BASSI mitume na ndugu waliokuwa katika Yahudi wakapata khabari ya kwamba watu wa mataifa nao wamelipokea neno la Bwana.


Roho akaniambia nifuatane nao, nisione mashaka. Ndugu hawa sita nao wakaenda pamoja nami, tukaingia katika nyumba ya mtu yule:


Ikawa kwa muda wa mwaka mzima wakakusanyika pamoja na kanisa na kuwafundisha watu wengi. Na wanafunzi waliitwa Wakristo kwanza hajio Antiokia.


Na wale wanafunzi, killa mtu kwa kadiri alivyofanikiwa wakaazimu kupeleka msaada kwa ndugu zao waliokaa Yahudi.


Nae akawapungia mkono wanyamaze, akawaeleza jinsi Bwana alivyomtoa katika gereza. Akasema, Enendeni, mkampashe Yakobo na ndugu zetu khabari hizi. Akaondoka, akaenda mahali pengine.


Walakini Wayahudi wasioamini wakawataharakisha watu wa mataifa na kuwatia nia mbaya juu ya ndugu.


WAKASHUKA wafu waliotoka Yahudi wakawafundisha ndugu ya kama, Msipotahiriwa na kuifuata desturi ya Musa hamwezi kuokoka.


Bassi, wakisafirishwa na Kanisa, wakapita kati ya inchi ya Foiniki na Samaria, wakitangaza khabari za kuongoka kwao Mataifa; wakawafurahisha ndugu sana.


Mtu huyo alishuhudiwa na ndugu waliokaa Lustra na Derbe.


Nao wakatoka gerezani wakaingia nyumbani mwa Ludia; na walipokwisha kuwaona ndugu wakawafariji, wakaenda zao.


Marra ndugu wakawapeleka Paolo na Sila usiku hatta Beroya. Walipofika huko wakaingia katika sunagogi la Wayahudi.


Marra hiyo wale ndugu wakampeleka Paolo aende zake kana kwamba anakwenda njia ya pwani; bali Sila na Timotheo wakashinda huko.


na wasipowakuta, wakamkokota Yason na baadhi ya ndugu mbele ya wakubwa wa mji, wakipiga kelele, wakisema, Watu hawa walioupindua ulimwengu wamefika na huku,


Paolo akazidi kukaa huko siku nyingi, kiisha akaagana na ndugu akatweka kwenda Shami; na Priskilla na Akula wakaenda pamoja nae, alipokwisha kunyoa kichwa chake katika Kenkrea; maana alikuwa ana nadhiri.


Na alipotaka kuvuka bahari aende hatta Akaya, ndugu wakamhimiza, wakamwandikia barua kwa wanafunzi wale wamkaribishe; nae alipofika akawasaidia sana wale waliokwisha kuamini kwa neema ya Mungu.


Tulipolika Yerusalemi ndugu wakatukaribisha kwa furaha.


Nao waliposikia wakamhimidi Mungu, wakamwambia, Ndugu yetu, unaona kwamba Wayahudi walioamini walivyo elfu nyingi, nao wote wana wivu sana kwa ajili ya torati.


Hatta tulipomaliza safari yetu kutoka Troa tukafika Ptolemai, tukawasalimu ndugu tukakaa kwao siku moja.


Kama kuhani mkuu nae anishuhudiavyo, na wazee wa baraza wote pia, ambao nalipewa barua nao kwa ndugu zao, nikaenda Dameski, illi niwalete wale waliokuwa huko hatta Yerusalemi, wamefungwa waadhibiwe.


Huko tukakuta ndugu, tukasihiwa nao tukae siku saba; na hivi tukafika Rumi.


baadae alionekana na ndugu zaidi ya khamsi mia pamoja; katika hao walio wengi wanaishi hatta sasa, wengine wamelala;


Na katika saa ile palikuwa na tetemeko la inchi, nalo kubwa, na sehemu ya kumi ya mji ikaanguka, wana Adamu elfu saba wakauawa katika tetemeko lile. Na waliosalia wakaingiwa na khofu wakamtukuza Mungu wa mbingu.


Lakini unayo majina machache, hatta katika Sardi, watu wasioyatia uchafu mavazi yao. Nao watakwenda pamoja nami katika mavazi meupe, kwa kuwa wamestahili.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo