Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 1:13 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

13 Hatta walipoingia, wakapanda orofani, walipokuwa wakikaa; Petro, na Yakobo, na Yohana, na Andrea, Filipo na Tomaso, Bartolomayo na Mattayo, Yakobo wa Alfayo, na Simon Zelote, na Yuda wa Yakobo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

13 Walipofika mjini waliingia katika chumba ghorofani ambamo walikuwa wanakaa; nao walikuwa Petro, Yohane, Yakobo, Andrea, Filipo na Thoma, Bartholomayo na Mathayo, Yakobo mwana wa Alfayo, Simoni Zelote na Yuda mwana wa Yakobo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

13 Walipofika mjini waliingia katika chumba ghorofani ambamo walikuwa wanakaa; nao walikuwa Petro, Yohane, Yakobo, Andrea, Filipo na Thoma, Bartholomayo na Mathayo, Yakobo mwana wa Alfayo, Simoni Zelote na Yuda mwana wa Yakobo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

13 Walipofika mjini waliingia katika chumba ghorofani ambamo walikuwa wanakaa; nao walikuwa Petro, Yohane, Yakobo, Andrea, Filipo na Thoma, Bartholomayo na Mathayo, Yakobo mwana wa Alfayo, Simoni Zelote na Yuda mwana wa Yakobo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

13 Walipowasili mjini Yerusalemu, walienda ghorofani kwenye chumba walichokuwa wakiishi. Waliokuwepo walikuwa: Petro, Yohana, Yakobo na Andrea; Filipo na Tomaso; Bartholomayo na Mathayo, Yakobo mwana wa Alfayo, Simoni Zelote na Yuda mwana wa Yakobo.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

13 Walipowasili mjini Yerusalemu, walikwenda ghorofani kwenye chumba walichokuwa wakiishi. Wale waliokuwepo walikuwa: Petro, Yohana, Yakobo, Andrea, Filipo, Tomaso, Bartholomayo, Mathayo, Yakobo mwana wa Alfayo, Simoni Zelote na Yuda mwana wa Yakobo.

Tazama sura Nakili




Matendo 1:13
45 Marejeleo ya Msalaba  

Yesu alipokuwa anaondoka kutoka huko akaona mtu amekeli fordhani, aitwae Mattayo, akamwambia, Nifuate. Akaondoka, akamfuata.


Nae mwenyewe atawaonyesha orofa kuhwa, imetandikwa tayari: huko tuandalieni.


Akamchukua Petro na Yakobo na Yohana pamoja nae, akaanza kufadhaika sana na kuhangaika.


Hatta alipokuwa akipita akamwona Lawi wa Alfayo, ameketi forodhani, akamwambia, Nifuate. Akaondoka akamfuata.


Wala hakumrukhusu mtu afuatane nae, illa Petro, na Yakobo, na Yohana ndugu yake Yakobo.


Hatta baada ya siku sita Yesu akawachukua Petro, na Yakobo, na Yohana, akawapeleka juu ya mlima mrefu kwa faragha peke yao:


Na mtu yule atawaonyesha orofa kubwa iliyopambwa; huko andalieni.


Bassi Tomaso, aitwae Didumo, akawaambia wanafunzi wenziwe, Twende na sisi, tufe pamoja nae.


Yuda akamwambia (siye Iskariote), Bwana, imekuwaje, ya kwamba wataka kujidhihirisha kwetu, wala si kwa ulimwengu?


Bassi yule kijakazi aliye mngoje mlango akamwambia Petro, Wewe nawe, je! huwi mmojawapo wa wanafunzi wake mtu huyu? Yeye akasema, Si mimi.


Simon Petro, na Tomaso aitwae Didumo, na Nathanael wa Kana wa Galilaya, na wana wa Zebedayo, na watu wengine wawili katika wanafunzi wake, walikuwa mahali pamoja.


Nae akawapungia mkono wanyamaze, akawaeleza jinsi Bwana alivyomtoa katika gereza. Akasema, Enendeni, mkampashe Yakobo na ndugu zetu khabari hizi. Akaondoka, akaenda mahali pengine.


Na bao walipokwisha kunyamaza Yakobo akajibu, akinena, Ndugu zangu, nisikilizeni,


Lakini Petro akasimama pamoja na wale edashara, akapaaza sauti yake, akawaambia, Enyi watu wa Uyahudi, na ninyi nyote mkaao Yerusalemi, jambo hili lijulike kwenu, mkasikilize maneno yangu.


Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe killa mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.


Palikiuwa na taa nyingi katika orofa ile walipokuwa wamekusanyika.


Bassi walipoona ujasiri wa Petro na Yohana, na kujua ya kuwa ni watu wasio elimu, wasio maarifa, wakastaajabu, wakawatambua ya kwamba walikuwa pamoja na Yesu.


Petro na Yohana wakawajibu wakawaambia,


baadae alionekana na Yakobo; tena na mitume wote;


Lakini sikumwona mtume mwingine illa Yakobo ndugu yake Bwana.


tena walipokwisha kuijua neema niliyopewa, Yakobo, na Kefa, na Yohana, wenye sifa kuwa ni nguzo, walinipa mimi na Barnaba mkono wa kuume wa shirika, illi sisi tuende kwa mataifa, na wao waende kwa watu wa tohara;


YAKOBO, mtumwa wa Mungu, na Bwana Yesu Kristo, kwa kabila thenashara zilizotawanyika, salamu,


MZEE kwa bibi mteule na watoto wake niwapendao katika kweli; wala si mimi peke yangu, bali na ndugu wote waijuao ile kweli;


YUDA, mtumwa wa Yesu Kristo, ndugu wa Yakobo, kwao waliopendwa katika Mungu Baba, na kuhifadhiwa kwa ajili ya Yesu Kristo baada ya kuitwa;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo