Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 1:11 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

11 wakasema, Watu wa Galilaya, mbona mmesimama mkitazama mbinguni? Huyu Yesu aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda juu mbinguni, atakuja jinsi hiyo hiyo mlivyomwona akienda zake mbinguni.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 wakasema, “Enyi wananchi wa Galilaya! Mbona mnasimama mkitazama angani? Yesu huyu ambaye amechukuliwa kutoka kwenu kwenda mbinguni atakuja tena namna hiyohiyo mlivyomwona akienda mbinguni.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 wakasema, “Enyi wananchi wa Galilaya! Mbona mnasimama mkitazama angani? Yesu huyu ambaye amechukuliwa kutoka kwenu kwenda mbinguni atakuja tena namna hiyohiyo mlivyomwona akienda mbinguni.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 wakasema, “Enyi wananchi wa Galilaya! Mbona mnasimama mkitazama angani? Yesu huyu ambaye amechukuliwa kutoka kwenu kwenda mbinguni atakuja tena namna hiyohiyo mlivyomwona akienda mbinguni.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 Wakasema, “Enyi watu wa Galilaya, mbona mnasimama mkitazama juu angani? Huyu Isa aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda mbinguni, atarudi tena jinsi hiyo hiyo mlivyomwona akienda zake mbinguni.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 wakasema, “Enyi watu wa Galilaya, mbona mnasimama mkitazama juu angani? Huyu Isa aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda Mbinguni, atarudi tena jinsi iyo hiyo mlivyomwona akienda zake Mbinguni.”

Tazama sura Nakili




Matendo 1:11
23 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa maana Mwana wa Adamu atakuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika zake; ndipo atamlipa killa mtu kwa kadiri ya kutenda kwake.


Amin, nawaambieni, Pana watu katika hawo wanaosimama hapa, ambao hawataonja mauti kabisa, hatta watakapomwona Mwana wa Adamu akija katika ufalme wake.


ndipo itakapoonekana ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni: ndipo mataifa yote ya ulimwengu wataomboleza, nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbingu kwa nguvu pamoja na utukufu mwingi.


Hatta atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote pamoja nae, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake:


Hapo ndipo watakapomwona Mwana wa Adamu akija mawinguni pamoja na nguvu nyingi na utukufu.


Punde kidogo wale waliohudhuria wakamwambia Petro, Hakika u mmoja wao, kwa sababu u Mgalilaya wewe, na usemi wako kama usemi wao.


Bassi Bwana, baada ya kusema nao, akachukuliwa juu mbinguni, akaketi mkono wa kuume wa Mungu.


Ndipo watakapomwona Mwana wa Adamu akija katika wingu kwa nguvu na utukufu mwingi.


Nao wakiingiwa na khofu na kuinama kifudifudi hatta inchi, wakawaambia, Kwa nini mnamtafuta aliye hayi katika wafu? Hayupo hapa, bali amefufuka.


Bassi nikishika njia kwenda kuwaandalia mahali, nitakuja tena, niwakaribisheni kwangu; illi nilipo mimi, nanyi mwepo.


hatta siku ile alipowaagiza kwa Roho Mtakatifu mitume aliowachagua, akachukuliwa juu:


akianza tangu ubatizo wa Yohana, hatta siku ile alipochukuliwa kwetu kwenda juu, lazima mmoja wao afanywe shahidi wa kufufuka kwake pamoja nasi.


Akiisha kusema haya, walipokuwa wakitazama, akainuliwa, wingu likampokea kutoka machoni pao.


akaonwa siku nyingi nao waliopanda nae kutoka Galilaya hatta Yerusalemi, na hao ndio walio sasa mashahidi wake mbele va watu.


Wakashangaa wote, wakastaajabu wakiambiana, Si hawa wote wasemao Wagalilaya?


Hatta Petro alipoona haya akawajibu watu, Enyi Waisraeli, mbona mnastaajabia haya, au mbona mnatukazia macho sisi, kana kwamba tumemfanya huyu aende kwa nguvu zetu sisi, au kwa utawa wetu sisi?


ambae ilimpasa kupokewa mbinguni hatta zije zamani za kufanywa upya vitu vyote, zilizonenwa na Mungu kwa vinywa vya manabii wake tokea mwanzo wa ulimwengu.


na kumugojea Mwana wake kutoka mbinguni, ambae alimfufua katika wafu, Yesu, anaetuokoa na ghadhabu itakayokuja.


Kwasababu Bwana mwenyewe atasbuka kutoka mbinguni na sauti kuu na sauti ya malaika mkuu, na panda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo, watafufuliwa kwanza;


kadhalika Kristo, akiisha kutolewa sadaka marra moja aziondoe dhambi za watu wengi, marra ya pili, pasipo dhambi, ataonekana nao wamtazamiao kwa wokofu.


Tazama yuaja na mawingu: na killa jicho litamwona, na hawo waliomchoma; na kabila zote za dunia wataomboleza kwa ajili yake. Naam. Amin.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo