Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Marko 9:9 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

9 Walipokuwa wakishuka mlimani akawaagiza wasimweleze mtu waliyoyaona, illa Mwana wa Adamu atakapokuwa amefufuka katika wafu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 Basi, walipokuwa wanashuka mlimani, Yesu aliwakataza wasimwambie mtu yeyote mambo waliyoyaona, mpaka Mwana wa Mtu atakapokuwa amefufuka kutoka kwa wafu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

9 Basi, walipokuwa wanashuka mlimani, Yesu aliwakataza wasimwambie mtu yeyote mambo waliyoyaona, mpaka Mwana wa Mtu atakapokuwa amefufuka kutoka kwa wafu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 Basi, walipokuwa wanashuka mlimani, Yesu aliwakataza wasimwambie mtu yeyote mambo waliyoyaona, mpaka Mwana wa Mtu atakapokuwa amefufuka kutoka kwa wafu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 Walipokuwa wakishuka kutoka mlimani, Isa akawakataza wasimwambie mtu yeyote mambo waliyoyaona, hadi Mwana wa Adamu atakapokuwa amefufuka kutoka kwa wafu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

9 Walipokuwa wakishuka kutoka mlimani, Isa akawakataza wasimwambie mtu yeyote mambo waliyoona, mpaka Mwana wa Adamu atakapokuwa amefufuka kutoka kwa wafu.

Tazama sura Nakili




Marko 9:9
15 Marejeleo ya Msalaba  

Hatateta, wala hatapaaza sauti yake; Wala mtu hatasikia sauti yake njiani.


Maana kama vile Yunus alivyokuwa siku tatu mchana na nsiku katika tumbo la nyamgumi, hivyo ndivyo Mwana wa Adamu atakavyokuwa siku tatu mchana na usiku katika moyo wa inchi.


Toka wakati huo Yesu akaanza kuwaonya wanafunzi wake ya kwamba imempasa kwenda Yerusalemi, na kuteswa mengi na wazee na makuhani wakuu, na waandishi, na kuuawa, na siku ya tatu kufufuka.


wakinena, Bwana, tumekumbuka kwamba yule mjanja alisema, alipokuwa hayi bado, Baada ya siku tatu nitafufuka.


Yesu akamwambia, Angalia, usimwambie mtu; illa enenda zako, ukajionyeshe kwa kuhani, utoe sadaka kama alivyoamuru Musa, iwe ushuhuda kwao.


Akawaagiza sana, mtu asijue khabari ile; akaamuru apewe chakula.


Akawaagiza wasimwambie mtu; lakini kwa kadiri alivyozidi kuwaagiza, ndivyo walivyozidi kutangaza khabari, wakashangaa mno kupita kiasi, wakinena,


Wakalishika neno lile, wakiulizana wao kwa wao, Huku kufufuka katika wafu maana yake nini?


Na marra hiyo walipotazama huku na huku, hawakumwona mtu, illa Yesu peke yake pamoja nao.


Akawaambia, Ndivyo ilivyoandikwa, na ndivyo ilivyompasa Kristo kuteswa, na kufufuka siku ya tatu;


Na sauti hii ilipokuja Yesu akaonekana peke yake. Nao wakanyamaza wasimwambie mtu siku zile neno lo lote la hayo waliyoyaona.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo