Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Marko 9:50 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

50 Chumvi ni njema; lakini chumvi ikitokwa na ladhdha yake, mtaitia nini ikolee? Mwe na chumvi ndani yenu, mkakae kwa amani ninyi kwa ninyi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

50 Chumvi ni nzuri, lakini ikipoteza ladha yake, itakolezwa na nini? Muwe na chumvi ndani yenu na kudumisha amani kati yenu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

50 Chumvi ni nzuri, lakini ikipoteza ladha yake, itakolezwa na nini? Muwe na chumvi ndani yenu na kudumisha amani kati yenu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

50 Chumvi ni nzuri, lakini ikipoteza ladha yake, itakolezwa na nini? Muwe na chumvi ndani yenu na kudumisha amani kati yenu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

50 “Chumvi ni nzuri, lakini ikipoteza ladha yake utaifanyaje ili iweze kukolea tena? Mwe na chumvi ndani yenu, mkaishi kwa amani, kila mmoja na mwenzake.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

50 “Chumvi ni nzuri, lakini ikipoteza ladha yake utaifanyaje ili iweze kukolea tena? Mwe na chumvi ndani yenu, mkaishi kwa amani, kila mmoja na mwenzake.”

Tazama sura Nakili




Marko 9:50
28 Marejeleo ya Msalaba  

Ninyi ni chumvi ya dunia: lakini chumvi ikiwa imeharibika itatiwani ikolee? Haifai tena kabisa, illa kufupwa nje na kukanyagwa na watu.


Wakanyamaza. Kwa maana walikuwa wakibishana wao kwa wao, ni nani aliye mkubwa.


Kwa sababu killa mtu atatiwa chumvi kwa moto, na killa dhabihu itatiwa chumvi kwa chumvi.


Kama yumkini, kwa upande wenu, mwe na amani na watu wote.


Khatimae, ndugu, kwa kherini; mtimilike, mfarajike, nieni mamoja, mkae katika imani; na Mungu wa upendo na amani awe pamoja nanyi.


Lakini matunda ya Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,


Neno lo lote lililo ovu lisitoke vinywani mwenu, bali lililo jema la kumfaa mwenye kuhitaji, liwape neema wanaosikia.


Lakini mwenendo wenu uwe kama inavyoipasa Injili ya Kristo, illi, nikija na kuwaona ninyi, au nisipokuwapo, niyasikie mambo yenu, kama mnasimama imara katika roho moja, kwa moyo mmoja mkiishindania imani ya Injili;


Bassi, kwa kuwa mu wateule wa Mungu, watakatifu na wapendwao, vaeni moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu,


Maneno yenu yawe na neema siku zote, yakikolea chumvi, mpate kujua jinsi iwapasa vyo kumjibu killa mtu.


mkawastahi sana katika upendo, kwa ajili ya kazi zao. Mwe na amani ninyi kwa ninyi.


Lakini zikimbie tamaa za ujana; nkafuate haki, na imani, na uaminifu, na upendo, na amani, pamoja na hao wamwitiao Bwana kwa moyo safi.


Fanyeni bidii kutafuta amani kwa watu wote, na utakatifu, ambao hapana mtu atakaemwona Mungu asipokuwa nao;


kwa maana ghadhabu ya mwana Adamu haiitendi haki ya Mungu.


Neno la mwisbo ni hili; mwe na nia moja, wahurumianao, wenye kupendana kama ndugu, wasikitikivu, wanyenyekevu;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo