Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Marko 9:29 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

29 Akawaambia, Namna hii haiwezi kutoka kwa neno lo lote, isipokuwa kwa kusali na kufunga.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

29 Naye akawaambia, “Pepo wa aina hii hawezi kutoka isipokuwa kwa sala.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

29 Naye akawaambia, “Pepo wa aina hii hawezi kutoka isipokuwa kwa sala.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

29 Naye akawaambia, “Pepo wa aina hii hawezi kutoka isipokuwa kwa sala.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

29 Isa akawajibu, “Pepo aina hii haiwezi kutoka isipokuwa kwa kuomba [na kufunga].”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

29 Isa akawajibu, “Hali hii haiwezi kutoka isipokuwa kwa kuomba na kufunga.”

Tazama sura Nakili




Marko 9:29
17 Marejeleo ya Msalaba  

Marra huenda, akachukua pamoja nae pepo wengine saba walio waovu kupita nafsi yake, nao huingia na kukaa humo; na mambo, ya mwisho ya mtu yule huwa mabaya kuliko ya kwanza. Ndivyo itakavyokuwa kwa kizazi hiki kilicho kiovu.


Yesu akawaambia, Kwa sababu ya kutokuamini kwenu. Kwa maana, amin, nawaambieni, Mkiwa na imani kama punje ya kharadali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa hatta kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu.


Lakini namna hii haitoki illa kwa kusali na kufunga.


Hatta alipoingia nyumbani, wanafunzi wake wakamwuliza kwa faragha, Mbona sisi hatukuweza kumfukuza?


Wakatoka huko, wakapita kati kati ya Galilaya: nae hakutaka mtu ajue.


Marra huenda, huchukua pepo saba wengine walio waovu kupita nafsi yake: nao huingia na kukaa humo: na mambo ya mwisho ya mtu yule huwa mabaya kuliko ya kwanza.


Na walipokwisha kuchagua wazee katika killa mji, na kuomba pamoja na kufunga, wakawaweka kafika mikono ya Bwana waliyemwamini.


bali nautesa mwili wangu na kuutumikisha; isiwe, nikiisha kuwakhubiri wengine, mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa.


kwa kazi na kusumbuka; kwa kukesha marra nyingi; kwa njaa na kiu; kwa kufunga marra nyingi; kwa baridi na kuwa uchi.


Kwa ajili ya kitu hiki nalimsihi Bwaua marra tatu kinitoke.


kafika mapigo, katika vifungo, katika fitina, katika kazi, katika kukesha, katika kufunga;


kwa sala zote na kuomha mkisali killa wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo, mkifanya juhudi sana, na kuwaombea watakatifu wote,


Na kule kuomba kwa imani kutamwokoa mgonjwa yule, na Bwana atamwinua; na kama amefanya dhambi, atasamehewa.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo