Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Marko 9:25 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

25 Nae Yesu akiona ya kuwa makutano yanakusanyika mbio, akamkemea yule pepo mchafu, akamwambia, Ewe pepo bubu ua kiziwi, mimi nakuamuru, mtoke, wala usimwingie tena.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

25 Yesu alipouona umati wa watu unaongezeka upesi mbele yake, alimkemea yule pepo mchafu “Pepo unayemfanya huyu mtoto kuwa bubu na kiziwi, nakuamuru, mtoke mtoto huyu wala usimwingie tena!”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

25 Yesu alipouona umati wa watu unaongezeka upesi mbele yake, alimkemea yule pepo mchafu “Pepo unayemfanya huyu mtoto kuwa bubu na kiziwi, nakuamuru, mtoke mtoto huyu wala usimwingie tena!”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

25 Yesu alipouona umati wa watu unaongezeka upesi mbele yake, alimkemea yule pepo mchafu “Pepo unayemfanya huyu mtoto kuwa bubu na kiziwi, nakuamuru, mtoke mtoto huyu wala usimwingie tena!”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

25 Isa alipoona kwamba umati wa watu wanakusanyika pamoja mbio, akamkemea yule pepo mchafu, akimwambia, “Wewe pepo bubu na kiziwi, nakuamuru umtoke, wala usimwingie tena!”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

25 Isa alipoona kwamba umati wa watu unakusanyika pamoja mbio, akamkemea yule pepo mchafu, akimwambia, “Wewe pepo bubu na kiziwi, nakuamuru umtoke, wala usimwingie tena!”

Tazama sura Nakili




Marko 9:25
17 Marejeleo ya Msalaba  

Wakati ule akaletewa mtu mwenye pepo, kipofu na bubu; akamponya, hatta yule kipofu na bubu akasema na kuona.


Yesu akamkaripia pepo, akamtoka; yule kijana akapona tangu saa ile.


marra makutano yote wakimwona wakashangaa wakamwendea mbio, wakamsalimu.


Marra baba yake yule kijana akapaaza sauti, machozi yakimtoka, akanena, Naamini, Bwana, nisaidie kutokuamini kwangu.


Akalia, akamrarua sana, akamtoka: akawa kama amekufa: hatta wengi wakasema, Amekufa.


Na Yesu alikuwa akifukuza pepo bubu. Ikawa yule pepo alipotoka, bubu akasema, makutano wakastaajabu.


Yesu akamkemea, akinena, Fumba kinywa, mtoke. Yule pepo akamwangusha katikati, akamtoka, asimdhuru.


Pepo wakawatoka wengi wakipaaza sauti zao wakisema, Wewe u Kristo, Mwana wa Mungu. Akawakemea, asiwaache kunena, kwa sababu walijua ya kuwa yeye ndiye Kristo.


Kwa sababu amemwamuru yule pepo mchafu kumtoka mtu yule. Maana marra nyingi amempagaa, nae akafungwa, akilindwa, na kufungwa minyororo na pingu, akavikata vile vifungo, akafukuzwa na yule pepo hatta jangwani.


Alipokuwa katika kumwendea, yule pepo akambwaga akamraruararua. Yesu akamkaripia yule pepo mchafu, akamponya yule mtoto, akamrudishia baba yake.


Akawa akifanya hayo siku nyingi. Lakini Paolo akakasirika akageuka akamwambia yule pepo, Nakuamuru kwa jina la Yesu Kristo, mtoke huyu. Akamtoka saa ile ile.


Lakini Mikael, malaika mkuu, aliposhindana na Shetani, na kuhujiana nae kwa ajili ya mwili wa Musa, hakuthubutu kumshitaki kwa kumlaumu, bali alisema, Bwana akukemee.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo