Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Marko 9:24 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

24 Marra baba yake yule kijana akapaaza sauti, machozi yakimtoka, akanena, Naamini, Bwana, nisaidie kutokuamini kwangu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

24 Hapo, huyo baba akalia kwa sauti, “Naamini! Lakini imani yangu haitoshi, nisaidie.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

24 Hapo, huyo baba akalia kwa sauti, “Naamini! Lakini imani yangu haitoshi, nisaidie.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

24 Hapo, huyo baba akalia kwa sauti, “Naamini! Lakini imani yangu haitoshi, nisaidie.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

24 Mara baba yake yule mvulana akapaza sauti akisema, “Ninaamini. Nisaidie kutokuamini kwangu!”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

24 Mara baba yake yule mvulana akapiga kelele akisema, “Ninaamini. Nisaidie kutokuamini kwangu!”

Tazama sura Nakili




Marko 9:24
21 Marejeleo ya Msalaba  

Yesu akamwambia, Ukiweza kuamini: yote yawezekana kwake aaminiye.


Nae Yesu akiona ya kuwa makutano yanakusanyika mbio, akamkemea yule pepo mchafu, akamwambia, Ewe pepo bubu ua kiziwi, mimi nakuamuru, mtoke, wala usimwingie tena.


Mitume wakamwambia, Bwana, utuongezee imani yetu.


akasimama nyuma karibu na miguu yake, akilia, akaanza kumchuruzia miguu kwa machozi yake, na kuipangusa kwa nywele za kichwa chake akibusu sana miguu yake, na kuipaka yale marhamu.


Akamgenkia yule mwanamke, akamwambia Simon, Wamwona mwanamke huyu? Naliingia nyumbani mwako, hukunipa maji ya kunawia miguu, bali huyu amenichuruzia miguu kwa machozi yake, na kuipangusa kwa nywele za kichwa chake.


Na Petro alikuwa akiyafikiri yale maono. Roho akamwambia, Wako watu watatu wanakutaka.


Kornelio, maombi yako yamesikiwa, na sadaka zako zinakumbukwa mbele za Mungu.


Maana katika shidda nyingi na dhiiki ya moyo niliwaandikieni nikitoka machozi mengi; si kwamba mhuzunishwe, bali mpate kujua upendo wangu nilio nao kwenu jinsi ulivyo mwingi.


Maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; na hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu:


Maana mmepewii kwa ajili ya Kristo, si kumwamini tu, illa na kuteswa kwa ajili yake,


Kwa hiyo twawaombea ninyi siku zote, illi Mungu wetu awahesabu kuwa nimeustahili wito wenu, akatimize killa haja ya wema na killa kazi ya imani kwa nguvu:


Imetupasa kumshukuru Mungu siku zote kwa ajili yenu, ndugu, kama ilivyo wajib, kwa kuwa imani yenu inazidi sana, na upendo wa killa mtu kwenu kwa wenzake umekuwa mwingi.


nikikumbuka machozi yako, illi nijae furaha;


Maana mwajua ya kuwa hatta alipotaka baadae kuirithi baraka, alikataliwa (maana hakuona nafasi ya kutubu), ijapokuwa aliitafuta sana kwa machozi.


tukimtazama Yesu, aliveianzisha imani yetu na kuitimiliza; ambae kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele zake aliuvumilia msalaba na kuidharau aibu, nae ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu.


Yeye siku hizo za niwili wake alimtolea yeye awezae kumwokoa na kumtoa katika mauti, maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi, akasikilizwa kwa sababu ya kicho chake;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo