Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Marko 9:23 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

23 Yesu akamwambia, Ukiweza kuamini: yote yawezekana kwake aaminiye.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

23 Yesu akamwambia, “Ati ikiwa waweza! Mambo yote yanawezekana kwa mtu aliye na imani.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

23 Yesu akamwambia, “Ati ikiwa waweza! Mambo yote yanawezekana kwa mtu aliye na imani.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

23 Yesu akamwambia, “Ati ikiwa waweza! Mambo yote yanawezekana kwa mtu aliye na imani.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

23 Isa akamwambia, “Ati, ‘Kama unaweza kufanya jambo lolote’? Yote yawezekana kwake yeye aaminiye.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

23 Isa akamwambia, “Kama ukiweza kuamini, yote yawezekana kwake yeye aaminiye.”

Tazama sura Nakili




Marko 9:23
12 Marejeleo ya Msalaba  

Akasema, Njoo. Petro akashuka chomboni, akatembea juu ya maji, illi kumwendea Yesu.


Yesu akawaambia, Kwa sababu ya kutokuamini kwenu. Kwa maana, amin, nawaambieni, Mkiwa na imani kama punje ya kharadali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa hatta kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu.


Amin, nawaambieni, Ye yote atakaenambia mlima huu, Ngʼoka ukatupwe baharini, asione shaka moyoni mwake, bali aamini kwamba hayo asemayo yamekuwa, yatamtukia hayohayo aliyosema.


Na marra nyingi amemtupa katika moto, na katika maji, amwangamize; lakini ukiweza neno, utuhurumie, utusaidie.


Marra baba yake yule kijana akapaaza sauti, machozi yakimtoka, akanena, Naamini, Bwana, nisaidie kutokuamini kwangu.


Bwana akasema, Mkiwa na imani kama punje ya kharadali, mngeuambia mzambarau huu, Ngʼoka ukapandwe baharini, nao ungewatiini.


Yesu akamwambia, Sikukuambia ya kwamba ukiamini utauona utukufu wa Mungu? Bassi wakaliondoa lile jiwe.


Mtu huyo alimsikia Paolo akinena; nae akamkazia macho akaona ya kuwa ana imani ya kuponywa,


Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu ampendezae Mungu lazima aamini kwamba yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo