Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Marko 8:35 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

35 Kwa maana atakae kuisalimisha roho yake, ataiangamiza, na mtu atakaeitoa roho yake kwa ajili yangu na kwa ajili ya injili, huyu ataisalimisha.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

35 Maana mtu anayetaka kuyaokoa maisha yake mwenyewe, atayapoteza, lakini mtu anayepoteza maisha yake kwa ajili yangu na kwa ajili ya Habari Njema, atayaokoa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

35 Maana mtu anayetaka kuyaokoa maisha yake mwenyewe, atayapoteza, lakini mtu anayepoteza maisha yake kwa ajili yangu na kwa ajili ya Habari Njema, atayaokoa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

35 Maana mtu anayetaka kuyaokoa maisha yake mwenyewe, atayapoteza, lakini mtu anayepoteza maisha yake kwa ajili yangu na kwa ajili ya Habari Njema, atayaokoa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

35 Kwa maana yeyote anayetaka kuyaokoa maisha yake atayapoteza, lakini yeyote atakayeyapoteza maisha yake kwa ajili yangu na kwa ajili ya Injili atayaokoa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

35 Kwa maana yeyote anayetaka kuyaokoa maisha yake atayapoteza, lakini yeyote atakayeyapoteza maisha yake kwa ajili yangu na kwa ajili ya Injili atayaokoa.

Tazama sura Nakili




Marko 8:35
27 Marejeleo ya Msalaba  

Na mtakuwa mkichukiwa na watu wole kwa ajili ya jina langu: lakini adumuye hatta mwisho, ndiye atakaeokoka.


Anaeipata roho yake ataiangamiza; nae anaeitoa roho yake kwa ajili yangu ataipata.


Maana mtu atakae kuisalimisha roho yake, ataiangamiza; na mtu atakaeitoa roho yake kwa ajili yangu, ataiona.


Na killa mtu aliyeacha nyumba, au ndugu waume, au ndugu wake, au baba, au mama, au watoto, au mashamba, kwa ajili ya jina langu, atapokea marra mia, na kurithi uzima wa milele.


Maana itamfaidia mtu nini kuupata ulimwengu wote akapata khasara ya roho yake?


Mtu ye yote atakaeisalimisha roho yake ataiangamiza, na mtu ye yote atakaeitoa ataihifadhi.


Kwa maana mtu akitaka kuisalimisha roho yake ataiangamiza, nae atakae kuitoa roho yake kwa ajili yangu, huyu ataisalimisha.


Lakini siyahesabu maisha yaugu kuwa kitu cha thamani kwangu kama kuumaliza mwendo wangu na khuduma ile niliyopokea kwa Bwana Yesu, kuishuhudia Injili ya neema ya Mungu.


Paolo akajibu, Mnafanyaje, kulia na kunivnnja moyo? kwa maana mimi, licha ya kufungwa tu, ni tayari hatta kuuawa katika Yerusalemi kwa ajili ya jina lake Bwana Yesu.


Maana nitamwonyesba mambo mengi makuu yatakayompasa kuteswa kwa ajili ya Jina langu.


Nami nafanya haya yote kwa ajili ya Injili nipate kuishiriki pamoja na wengine.


Kwa hiyo napendezwa na udhaifu, na maumivu, na dhiiki, na adha, na shidda, kwa ajili ya Kristo. Maana niwapo dhaifu ndipo nilipo ua nguvu.


Bassi usiutahayarikie ushuhuda wa Bwana wetu, wala mimi mtumwa wake, bali uvumilie mabaya pamoja na Injili kwa kadiri ya nguvu ya Mungu;


Wanawake walipokea wafu wao waliofufuliwa: na wengine walibanwa, wasiukubali ukombozi, wapate ufufuo ulio bora:


Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; wala hawakupenda maisha yao hatta wakati wa kufa.


Usiogope mambo yatakavokupata: tazama mshitaki atawatupa baadhi yenu gerezani illi mjaribiwe, nanyi mtakuwa na mateso siku kumi. Uwe mwaminifu hatta kufa, nami nitakupa taji ya uzima.


Nikamwambia, Bwana wangu, wajua wewe. Akaniambia, Hawo ndio wanaotoka katika shidda ile iliyo kuu, nao wamefua mavazi yao wakayafanya meupe katika damu ya Mwana Kondoo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo